STORY YA KWELI YA MAISHA YANGU

15:01:00 Unknown 1 Comments



Nilibahatika kumpata binti mmoja ambaye tulikaa naye kwa zaidi ya miaka mitatu kuanzia mwaka wa pili chuoni mpaka mwaka mmoja baadae tukiwa mtaani.

Alinipenda sana nami nilimpenda ingawa kuna baadhi ya mambo nikawa namkosea na akawa akinishauri niachane na mambo hayo bila ya mimi kuonesha dalili za mabadiliko.

Baadhi ya mambo aliyokuwa akiyachukia ni kama vile ulevi kwa kupindukia,uvutaji sigara na kutokuwa makini na matumizi ya pesa zangu na kuna mara moja au mbili alinifuma na baadhi ya mabinti na kunisamehe.

Tulipendana sana na alinidekeza na kiukweli nililiona hilo na sasa likanifanya niwe na kiburi na kuanza kumdharau, kumpiga na hata kutokumjali.

Pamoja na kumpiga na kumdharau kote huko na kujionesha live kuwa simpendi yeye alizidi kunipenda, mbaya zaidi kuna siku kwa kuwa tulianza kukaa pamoja kila mmoja akiwa na kazi yake basi nikamwacha akiwa anaumwa na kwenda kwenye pombe.

Nilirudi na kuambiwa kuwa yuko hospital lakini sikwenda mpaka siku ya pili yake bila kujua angeishije au anaendeleaje huko.Alifanikiwa kutoka salama baada ya siku tatu na tatizo alikuwa na vidonda vya tumbo na nyinikizo la damu.

Alikaa na kunisihi kwa mara ya mwisho kuwa kama sibadiliki basi yeye angeniacha na kuendelea na maisha yake lakini bado nikawa sisikii tena zaidi ya kuwa jeuri kwani nilijua ananipenda na hata akikosea nikiwa mkali basi yeye huniomba msamaha.

Siku moja asubuhi nikiwa naamka nikaona akiwa anapanga nguo zake na mimi sikujali nikajua hata kama ataondoka atarudi tena kwani ananipenda sana. hivyo mimi nikaondoka na kwenda zangu mitaani.

Nilirudi na kukuta kaondoka na kila kilichochake na kaniachia ujumbe mfupi usomekao:

Hello Mark,

Nimejaribu kukuvumilia na kuamini kuna siku utabadilika, lakini kilichoendelea ikawa kwa mimi kuzidi kuumia na kufikia hatua ya kupatwa na maradhi yasababishwayo na huzuni.

Wakati huu naondoka nikiamini sitarudi tena na ninakutakia maisha mema na kukuomba ubadilike kwani hakuna atakayekuweza na kukuvumilia kama nilivyofanya.

Kumbuka "UTAUTAMBUA UMUHIMU WA MAJI PALE VISIMA VIKIKAUKA"

Maisha mema

Faraja

Niliusoma ule ujumbe na kutabasamu nikiamini kuwa atarudi tu nami nikaendelea na maisha yangu.

Leo hii ni mwaka wa pili Faraja hajarudi na nilipata taarifa na kumshuhudia akiwa na mtu mwingine na hatimaye kuishuhudia harusi yake.

Anaishi maisha mazuri na mmewe na kila mtu anamsifia yule kijana kuwa kapata bahati ya mke bora.. nimekuwa naumia kila nikimwona na yule kijana na napatwa na wivu na sina njia zaidi ya kulia kila kukicha.

Mpaka sasa nimekuwa na  uhusiano na mabinti zaidi ya kumi na mbili tofauti na sijamwona atakayeniweza na sasa nimekuwa kama nimechanganyikiwa na siwezi kukaa na mtu tena.

Leo nakuja kutambua kuwa kile nilichokuwa nikikidharau kumbe ilikuwa ni almasi na sasa wengine wanafurahia uwepo wake.

Kwa kila mtu aliye kwenye mahusiano aangalie ni kwa jinsi gani anafanya mambo ambayo ni hatari kwa kuharibu uhusiano na kamwe usije kumpata kama uliyenaye sasa.

Comment Nakupenda Mpenzi wangu kama unaye na unamjali kisha share kwenye wall yake tuone kama huna mchepuko hapa fb :)

You Might Also Like

1 comment: