Kanga moja yazua balaaa

18:03:00 Unknown 0 Comments

Kuna nyumba ya mlevi mmoja nje kuna shimo kubwa la maji bila
mfuniko.

Siku moja karudi usiku kalewa tooooop, mambo yakawa hivi:

MUME: Fungua mlango!
MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.
MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.
MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!.

(MUME akachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo dubwi!
MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani
na kumfungia mke nje.)
MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.
MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka wapi usiku huu na
kanga moja

You Might Also Like

0 comments: