Laini ya simu leo ndio itatoa hitimisho la ndoa yangu
Sikuwahi kuwa na ugomvi na mke wangu mpaka
pale tulipoanza kukaa nae mapema mwaka huu.
Na ugomvi wetu mkubwa ulikuwa ni kwenye meseji alizokuwa akizikuta katika simu yangu mara
kwa mara kutoka kwa mpango wa kando bongo twaita totoz.
Kuna wakati kila niliporudi toka matembezini hasa nyakati za usiku ilinibidi kuificha simu yangu
kwenye gari mara, kabatini mara sebuleni mara chumba cha wadogo zangu lakini kwa kuwa nina tatizo la usingizi mzito mara nyingi nilishtushwa
na mangumi baada ya kuwa kaisaka na kuipata na kuwa amezisoma sms zote.
Ile hali ilininyima raha sana na ikanibidi nianze kujifunza mbinu mpya kama vile kuweka
password kwenye simu lakini alichomoa laini na kuiweka kwenye simu nyingine na kupokea sms
pia.
Sasa nikafanikiwa kuipata hii mpya ya kuweka namba ya siri kwenye laini na simu pia lakini nayo
haikufua dafu kwani kila siku nilienda kurenew laini baada ya kuzijaribu password na kisha
zikajiblock.
Kwa kuwa nina mademu wengi nikaanza kukonda na hata kuwakimbia maana ikawa inaleta shida kwangu.
Miezi michache iliyopita rafiki mmoja akanipa trick ya kuwa na lain ya bandia na ambayo naiweka
kwenye simu nikifika home na ile yangu naiweka mfukoni hivyo sms haziingii kwani watu wanakuwa hawaijui kabisa.
Njia hii imekuwa kiboko kwani zaidi ya miezi miwili hatujagombana mpaka akanisifia kuwa nimekuwa mme mwema sasa nami nikamwambia asipate tabu mie ni wake daima.....
Sasa jana kuamkia leo nikaenda club pale THE GREEN LOUNGE kupata mziki bomba kutoka kwa
DJ KIZZU na kweli nimekunywa sana na kujirusha na totoz, usiku nikarudi na kubadili laini kama
kawa na nikalala.
Naamka muda huu ile suruali imefuliwa na kumuuliza dada wa kazi akasema iliyeifua ni wife
na kuwa ile laini aliichukua na kuweka kwenye simu na kuondoka nayo kwenda kazini.
Hapa akili imesizi maana sipati picha kuna watoto wachuo niliwapa namba yangu jana na leo
nilitakiwa niwatoe out na sijui wataandika nini na sms gani mpya zitakuwepo sasa.....
Kichwa hakipo sawa maana naona leo wife atarudi kavimba na yaweza kuwa vita zaidi ya ile ya kossovo
0 comments: