Mambo ya ajabu afanyayo kuku
Kuku ana tabia moja ya ajabu sana. Ukimmwagia
mchele yeye atazidi kula punje moja moja huku
akiparua zaidi mpaka chini na mchele mwingine
akiutupia nyuma.
Yeye haamini kama hapa juu uko hivi basi pengine chini uko safi na mzuri zaidi.
Kuku huyu ni mfano wa baadhi ya sisi vijana ambao tuko makazini na tuna nafasi zetu lakini bado tunataka kugombania majukumu ya
wenzetu kwa ajili ya ulafi wa nafsi zetu.
Kwa nini mtu usiamue kuridhika kwa kile ulicho
nacho na kujituma kwa bidii ukitegemea mema
zaidi baadae?
Au tunasahau mtaka mengi kwa pupa hukosa yote
au huambulia aibu?
Kwa wewe mwenye kujituma na kuheshimu nafasi yako na ya mwenzako katika kila jambo naomba nikupe heshima na kukutakia siku njema
0 comments: