NI wangapi leo pamoja na umaarufu wetu twawakumbuka wazazi wetu??

11:43:00 Unknown 0 Comments




Kulikuwa na kijana mmoja ambaye alikuwa akiishi na mama yake mzazi tuu baada ya baba yake kufariki na familia yao ilikuwa ya kipato cha chini sana.

Kijana alikuwa ni mzuri wa sura, tabia na pia alikuwa na akili sana ingawa mama yake kila siku alionyesha kuhuzunika sana.

Siku moja yule mtoto akamuuliza mama yake, “Mama, kwa nini kila mara unaonyesha uso wa huzuni?" Mama akamjibu, “ Mwanangu, kuna mzee mmoja wakati nikiwa kijana aliwahi kuniambia mtu mwenye meno kama yako huja kuwa mtu maarufu sana.”

Mtoto akauliza tena, “Mama hautapenda mimi nije kuwa mtu maarufu?”

“Sio hivyo mwanangu! Ni mama wa aina gani ambaye hatapenda mwanae kuwa mtu maarufu na anayeheshimika? Nina huzuni siku zote kwa kuwa najua ukiwa maarufu utaniacha hapa na kuwa busy na watu wengine.”

Baada ya mtoto kusikia hivyo akaanza kulia kwa uchungu mbele ya mama na kukimbia kwenda nje ambako akachukua jiwe na kuyapiga meno na jino moja likadondoka chini na kumwacha akitokwa na damu nyingi sana.

Mama alipoenda nje alishangaa kumwona mtoto kajipiga na mdomo unatoa damu na jino moja halipo.

Akamuuliza, “Kwa nini umeamua kufanya hivyo?”

Akajibu, "Mama kama meno haya yatanifanya kuwa maarufu na kukusahau ni bora niyatoe na kubaki bila umaarufu wowote ule, Sitaki kuwa maarufu kwa watu na nikakusahau nataka kuwa maarufu kwa kukusaidia wewe MAMA na kupata BARAKA ZAKO"

NI wangapi leo pamoja na umaarufu wetu twawakumbuka wazazi wetu??


Like page hii Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: