Nimemkosa mtoto na ananiona mie mbulula

07:22:00 Unknown 0 Comments

Sikuwahi fikiria kama kuna siku ningefanikiwa
kumpata mtoto mwenye uzuri, umbo na rangi
kama ile kabisa maishani mwangu lakini
yamenikuta.
Juzi nikiwa natoka zangu town mnyaki nature
rafiki yangu wa ukweli akanipigia simu kuwa yupo
maeneo ya nyambono na kuniambia nikamcheki
mara moja kwa ajili ya lunch.
Nikiwa njiani nikamng'aza bibie mmoja mwenye
swaga za kudatisha na hatimaye akaniteka
taratibu.
Nikashuka kwenye daladala na kumfuata na
kumpa mwaliko wa lunch akasita sita ila kutokana
na kusisitiza kwangu hatimaye wote tukaelekea
nyambono.
Baada ya kufika nyambono Bar nikamkuta
Suphian na kama kawaida yetu story zikaanza
pale huku bia zikishuka kwa fujo na binti taratibu
akawa kaanza kuyakubali mapigo huku akiwa
anamtafuna ndege mmoja maarufu kwa jina la
kuku.
Si wajua tena vijana wa sasa pale kila simu
iliyoingia iliongelea fedha tu na lengo kumfanya
mtoto azidi kudata.
Meza ya jirani karibu na mlango walikuja na
kukaa majamaa fulani ambao sikutaka
kuwafuatilia sana ila ukiona vifua vyao lazima
ujue wananyanyua vyuma au matairi ya trekta.
Baad ya kufurahi pale tukaamua tuhame kiwanja
twende pande mpya.
Tukawasha gari la suphian na kwenda mitaa ya
mbalizi. Na tukaendeleza bia mwendo mmoja.
Haikupita dakika chache gari moja ikapaki pale na
wale majamaa tuliokaa nao meza ya jirani kule
bar wakashuka pale.
Mmmmh mie machale yakaanza kunicheza
nikamwambia jamaa tuondoke nimeona kama
twafatiliwa vile. Ingawa naona binti kama
hashtuki vile
Ile twataka kusimama tu jamaa wakaja na kusema
hatoki mtu hapa.
Mimi nikaanza kutetemeka pale lakini jamaa wale
wakasema msijali wakaagiza bia, mie nikaanza
kuhofia nisije wekewa sumu pale lakini wale
jamaa wakaniita nje na kusema kaka yaani wewe
kula pombe usijali....tunafuraha sana tulitaka
tujue nani anatembea na dada yetu maana tangu
aambukizwe UKIMWI watu wamekuwa
wakimkimbia na yeye anakosa raha kwani hana
mtu hivyo wewe ni shujaa.
Jasho la uoga wa kifo likaanza kunitoka upya na
safari hii ni hili la NGOMA, nikamwita suphiani na
kumwambia kuwa kumbe hawa ni kaka wa binti
na wanadai binti kawaka........tukatafuta upenyo
na kuwakimbia.
Nusu saa baadae yule binti akatupigia mbona nyie
sio wastaarabu? Yaani mmenileta mbalizi na
kuniacha na hawa jamaa zenu kulikoni?
Baada ya kuongea nae na kumwelewesha kuwa
walidai kuwa ni kaka zake binti akacheka na kudai
duniani akili wale mlipoondoka wakaanza kunipa
sound wananitaka pia.......sio kaka zangu ila
wamewazidi ujanja.
Nimeishiwa nguvu naona majanga hayaniishi...
Sasa mtoto nimemkosa na ananiona mie mwoga

Comment hapa

You Might Also Like

0 comments: