Wanandoa wawili wanusurika kuzama baharini
Kuna wanandoa wawili ambao walikuwa wanatoka fungate lao walilofanyia katika kisiwa kimoja
ambapo walitumia mtumbwi kwenda huko.
wakiwa katika mtumbwi wao wanasafiri kurudi nchi kavu, ghafla mawimbi makubwa yenye nguvu yakaanza kuupiga ule mtumbwi.
Yule mme akawa anaogopa huku kakaa kimya bila kuongea neno na mkewe akawa anapiga kelele za hofu kubwa.
Mke akamuuliza mbona wewe umekaa kimya, kwani wewe hauogopi? Haujui kuwa leo inaweza kuwa mara yetu ya mwisho kuwa pamoja? maana kwa mawimbi haya
hatuwezi kupona labda iwe ni kwa muujiza......... Jamani mbona hujibu? Wakati wote huo yule mme akikuwa kakaa kimya
Ndipo mme akachukua kisu chake chenye makali na kukisogeza karibu na shingo la
Mkewe na wakati wote huo yule mke alikiwa akishangaa, kwa sauti ya chini akauliza unataka
kunifanya nini na kisu hicho shingoni mwangu?
Mme akamuuliza kwani wewe haugopi?
Mke akajibu,"Siogopi kwani najua huwezi fanya kitu na kisu hicho, kwanza kipo mkononi mwa mtu anipendaye"
Mme akakirudisha kile kisu chini na kumwambia mkewe,"Nami siogopi juu ya mawimbi haya kwani najua yapo mkononi mwa MUNGU na ananipenda"
Hivyo chochote kitakachotokea hakitakuwa na madhara kwetu kwani MUNGU ndiye atakaye toa amri ya mwisho na itatendeka
kwa mapenzi yake bila kutuathiri sisi.
Funzo
Ukimtegemea MUNGU katika mipango yako kamwe hakuna wa kukurudisha nyuma.
Nawatakia weekend NJEMA
0 comments: