Wapende wazazi wako wakiwa hai

10:32:00 Unknown 0 Comments




Kijana mmoja alikuzwa na mama yake ambaye alikuwa na jicho moja huku moja likiwa chongo.

Mama huyu alikuwa masikini wa kutuptwa na ili amfanye mwanae aishi kwa furaha, ilimbidi aajiriwe na shule ya jirani awapikie wanafunzi na baadhi ya waalimu ili aweze kujikimu.

Watu wengi hasa wanafunzi walimcheka sana yule mama na kumtania yule kijana jambo lililomfanya amchukie sana mama yake kwa kuwa na jicho moja.

Kuna wakati yule kijana alimfuata mama yake na kumwambia alitamani mama yule afe au hata kijana pia afe kwani mama yule alikuwa fedheha kubwa kwake.

Baada ya kuhitimu mafunzo kijana alihama mji na kwenda mbali akapata kazi, akaoa na kuwa na watoto.

Kwa kuwa hakumkumbuka mama wala kumwambia yuko wapi, mama alimsaka mpaka siku akafika nyumbani kwa yule kijana wake wa pekee.

Wajukuu zake walipomwona walimcheka sana na kijana alipopigiwa simu kuambiwa kuna mgeni yeye akatoa amri kuwa yule mama asiingie ndani na kutimliwa.

Miezi michache baadae lile darasa ambalo lilikuwa linapikiwa na yule mama wakaamua kufanya paty ili wakumbushie enzi zao na wote wakasafiri na wakakusanyika pale shuleni kwao kwa zamani.

Kijana nae akamdanganya mkewe kuwa anaenda kwenye biashara muhimu, alipofika kule watu wakamwambia mama yake amefariki mwezi mmoja uliopita na yeye hakuumia hata chembe......ila wakasema kuna barua aliiacha na alisema ukija tukupe....

Barua ilisomeka:

Mwanangu kipenzi,

Ninakukumbuka sana na nitaendelea kukukumbuka kila wakati.

Nisamehe kwa kuwa nina jicho moja na jingine likiwa chongo, na hasa nilivyowatishia watoto wako kwa kuwa na jicho moja.

Nilifurahi kusikia wewe na marafiki mtakuja katika shule yenu mliyosoma huku nikiwapikia, ila naumia kwani nitashindwa kunyanyuka hapa kitandani na hata kuja kukuona kwani kwa homa hii naweza kufa kabla sijakuona mara ya mwisho.

Nisamehe kwa jinsi nilivyokuwa kero kwako wakati unakua kutokana na jicho langu moja kuwa chongo.

Wakati ukiwa mdogo ulipata ajali ya gari ukiwa nami na jicho lako likaharibika nami nikaamua kukupa jicho langu kwa kuwa wewe ni furaha yangu.

Kila siku nilifurahi kukuona ukiwa una macho yako yote mawili na naufurahia ule uamuzi wangu.

Nitakupenda daima

Mama yako 

Funzo

Hakuna kama mama

Wapende wazazi wako wakiwa hai

Mama zetu wanatuvumilia katika mengi, hata angeamua kukutupa chooni usingekuwepo hapo ulipo

Mapungufu yetu madogo na makubwa katika miili yetu walipigania na kuyafuta na kutufanya tuwe leo hivi

Una kila sababu ya kuandika "Asante MUNGU kwa kunipa WAZAZI"

Comment HAPA

You Might Also Like

0 comments: