Demu mwingine wa facebook asababisha nivimbe uso na kuipukutisha akaunti yangu benki
Niliwahi zangu home nikafika mida kama ya saa moja kasoro hivi, basi moja kwa moja nikapitiliza zangu mpaka kwenye kafriji kangu na kushangaa kuiona grants nikajiuliza niliiweka mida gani tena???
Kwa raha zangu nikajisogeza mpaka sebuleni na kuwasha laptop yangu nikaiunga na net na taratibu nikaanza kuchati facebook huku natupia glasi ya grants.
Nikaja onana na mrembo mmoja ambaye nimekuwa namsumbua sana kwa kumtaka awe mpenzi wangu ila yeye akawa anadai ana bwana yake lakini mimi nikamsisitiza aachane nae kwani mimi nitampa good life.
Kitu cha grants kikanipa ujasiri nikamwambia mtoto sasa leo nimekuona mtandaoni basi tuonane... akaniambia no hata weza mme wake anaweza tokea.. nikamwambia achana nae wewe niambie uko wapi nije, baada ya mabishanomarefu hatimaye kidume nikashinda na akaniambia niende mitaa ya town karibu na isimike atakuwa pale maana ndio maskani yake.
Kwa furaha nikagugumiza grants yote na kuwasha gari langu kisha nikaanza safari ya kwenda town kuonana na mtoto aliyenisumbua kwa muda mrefu bila majibu. Nikawa najisemesha kuwa leo atakoma kuringa.
Nikafika na kumkuta pale nje akaniambia kwanza ana kaka zake wanatakiwa kwenda uyole then tukiwapeleka tutakuwa free kabisa yaani kwa raha zetu nikitaka hata nimrudishe weekend...moyoni nikajisemesha "mwee kunoga"
Kijana nikawachukua mpaka benki na kuchukua balance ya laki na kuweka zangu mafuta kiasi kisha tukaanza kwenda uyole.
Njiani demu akadai anataka ajisaidie mara moja hivyo nikasimamisha gari na katika hali ya kushoo samu lavu nikashuka ili niwe mwangalizi asije pata majanga (si wajua tena ukiwa na mali mpya ulinzi muhimu kuongeza credits)
Mara nikaona na ule mlango wa kaka yake unafunguka sikushangaa sana nikajua tu itakuwa ule msemo usema, "katika kundi la mbuzi mmoja akikojoa wote hukojoa"
Lakini cha kushangaza akaingia na kulizima gari na kutoa ufunguo na nikaona hakuna cha kujisaidia yule binti wala nini. Nikaanza kuhisi kuna tamthilia inataka kuanza kupitia lunginga isiyo sahihi, lakini nikapiga moyo konde.
Mara jamaa akaniambia, "Oya kidume sogea hapa, wewe ndio fundi wa kutongoza wake za watu FB na mbaya zaidi unaniponda sana, eti mimi kapuku sina hela????????"
Kabla sijajibu nikala kibao, mtama, teke na ngumi vikaja kwa pamoja,na kwakuogopa watu wasije nikawa najifanya kucheka tu pale lakini ki ukweli ngumi zilikuwa ninaniingia na wakati huo ile grants ikawa imeisha.Ila maumivu ya ngumi yakabadili nafasi ya alcohol
Wakaninyanyua juu juu na kunitupa siti ya nyuma ya gari mpaka uyole na kunipeleka sehemu nami nikanawa kutoa damu kisha tukaingia bar na wakaalika watu kibao.
Wakanza kunywa mie nikagoma, akataka anipe nakozi ikanibidi nami niombe tu grants. Tukanywa sanapale tukiwa na jamaa zao na bili ilipokuja wakaniletea mimi.
Bili ya vinywaji pale ilikuwa imefikia laki 300,000 na wakasema nilipe, pale nikawa na 70,000 tu, ikanibidi niombe twende benki wakakataa nikakumbuka kuwa kwenye simu kuna hela ya kulipa pango la nyumba ambalo nilitakiwa kulipa siku ya pili asubuhi.. nikawarushia.
Kutoka pale tukaja mjini tukaingia kama baa nne mpaka wakahakikisha sina hata senti wakanipa gari na onyo kali nami nikajivuta mpaka mitaa ya home.
Usiku ule nyumbani hakuna aliyegundua lakini asubuhi baada ya kuona jinsi uso ulivyovimba wakaniuliza mbona jana nilichellewa kuliko kawaida na kwanini nimevimba vule?? Sikuwa na jinsi ikanibidi niwadanganye kuwa nilikuwa napigana na vibaka waliotaka kunipora gari.
Nikatoka pale na kuanza mtafutano na mama mwenye nyumba maana mshara wangu wote niliumaliza kwa wale mabaunsa na benki sikuwa na balance tena.
Mpaka sasa nimebadili akaunti ya facebook na sitaki tena kuchati na wadada na nashukuru uso wangu unaendelea vyema
Haya ndio majanga yaliyonikuta mwisho wa mwezi
Umeipenda hadithi hii? kama ndio comment funzo lake HAPA
0 comments: