Soma jinsi kipofu aliyefanikiwa kumuongoza mwenzake

23:06:00 Unknown 0 Comments





Vijana wawili walilazwa katika hospital moja kwa magonjwa tofauti.

Kijana wa kwanza alikuwa kalazwa kitanda karibia na dirisha na yule kijana mwingine alilazwa upande wa pili wa dirisha mbapo asingeweza kuona mambo yanayoendelea nje ya dirisha.

Yule aliyelala mbali na dirisha alikuwa anaumwa na hawezi kusimama wala hata kujigeuza na yule upande wa dirishani yeye angalau alijiweza.

Kila siku baada ya kupata dawa na chakula majira ya mchana yule mgonjwa wa dirishani alipenda kuamka na kwenda kukaa dirishani na kumsimulia mwenzake mambo mazuri yaliyokuwa yakiendelea huko nje.

Alikiwa akimsimulia jinsi kulivyo na bustani nzuri pembezoni mwa mto na ambavyo watoto, watu wazima na hata vijana wenye wapenzi walivyolitembelea eneo lile na kuonyesha jinsi walivyolifurahia eneo lile.

Ilikuwa ni kawaida yake kila siku yule mgonjwa wa dirishani kumsimulia mwenzake na hakika mwenzake alifurahi sana kwani hakuweza kabisa kuona kutokana na kubanwa na homa mpaka kushindwa kujigeuza.

Siku ziliendelea na hatimaye siku moja yule mgonjwa wa kitanda cha dirishani akafariki.

Yule mgonjwa wa upande wa pili akamuuliza nesi, "huyu mwenzangu yuko wapi mbona tangu jana sijamsikia sauti yake akinisimulia jinsi watu wanavyootea jua?"

Nesi akamwambia, "Pole sana huyu mwenzako kwa bahati mbaya kafariki"

Mgonjwa alihuzunika sana na kuomba aamishiwe kile kitanda na kulazwa kile kitanda cha dirishanio na kuzidi kuumia kwa nini amefariki mapema vile kwani alipenda hadithi zake.

Siku zikaenda nae akapata nafuu na siku moja akafanikiwa kutazama nje ya dirisha na kuona mambo yako tofauti na vile alivyokuwa akisimuliwa na yule mwezake.

Akaamua kumuuliza , mbona "yule mwenzangu alinisimulia mambo mengi yaliyokuwa yakiendelea kupitia hapa dirishani na kusema kuwa kuna mto na ufukwe lakini sioni au nimehamishwa?"

Yule nesi akamwambia , "pole sana mbona yule alikuwa kipofu? Aliongea hivyo kukupa nguvu na faraja ili usijione kama wewe u mgonjwa sana na uweze kuifanya akili yako kuwa huru na ya furaha kidogo'

Yule mgonjwa alilia sana na kumkumbuka yule mgonjwa na kutamani laiti angemwona ampe asante kwani alimfanya apate faraja na kuona msaada kwake na kwamba alikimbuka alivyokuwa akisubiri kwa hamu muda wa kusimuliwa.

Je na wewe unamsaidiaje/wasaidiaje wenzako ili waone umuhimu wa kuwepo kwao hapa duniani pamoja na shida walizonazo?

Jibu zuri natoa zawadi

Kumbuka kusharena ku-comment kwa kubofya Hapa

You Might Also Like

0 comments: