Ha ha ha ha rafiki wa fuledi aambulia yai kwenye matokeo

20:29:00 Unknown 0 Comments

Hi Fuledi

Mimi ni binti ambaye matokeo yetu ya kidato cha yametoka leo, pamoja na kuwa nina maumivu makubwa sana baada ya kujikuta nipo kwenye kundi kubwa la wenzangu na mimi tuliopata DIV zero naomba niwaombe radhi wazazi na marafiki zangu wote bila kumsahau baby wangu.

Msema ukweli ni mpenzi wa mungu, mie nina account humu fesibuku, na pia nina marafiki zaidi ya 5000 na followers kibao.

Kweli nilifurahia maisha kwani nikipost tu kitu natumia masaa mengi kujibu comments na pia nikiweka picha nibalaaa maana nitajibu comments na pia kwenda inbox kujibu sms ambazo marafiki hasa wa kiume wamenitumia na wengine kunitaka nitoke out.

Kweli kazi niliwaonyesha na ikafika kipindi sehemu zote maarufu nazipata na naomba hela ya tuition kumbe nanunulia kifurushi cha internet na kwenda kupigia picha studio.

Hivi sasa nina zero nimejaribu kuuliza wanasema siwezi hata kupata kazi ya ulinzi na hata kuwa model siwezi kwani kiingereza changu ni kile cha kujibu comments yaani cha kifesibuku

Nisaidieni nifanyaje maana nimechanganyikiwa naona hata aibu kuonekana kitaaa

Like Tabasamu na Fuledi soma maoni ya wadau Hapa

You Might Also Like

0 comments: