Habari ya kusikitisha!!!! Mama wa ajabu aliyempenda mwanae hata baada ya kufa
Mama mmoja alilazwa hospitali akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa maumivu makali kichwani na alikuwa katika hali mbaya sana.Mwanae wa pekee pamoja na baadhi ya ndugu walikizunguka kitanda cha mama wakijitahidi kumpa msaada wa karibu wakishirikiana na wauguzi.
Muda mchache baadae yule mama akafa kwa kuzidiwa na homa na mwanae alilia sana kiasi cha kukosa nguvu huku ndugu wakimsaidia.
Siku ya pili kijana yule akarudi nyumbani na kufungua kabati la mama yake ili apange vitu vizuri na kuona kuna dawa zimewekwa na barua pembeni yake.
Ile barua iliandikwa, " Chuukua hizi dawa mwanangu kipenzi na uzinywe, najua mwili wako utakuwa na baridi na homa baada ya kunililia sana"
Mapenzi ya mama ni mapenzi ya kweli kwetu sisi hata kama hatuko nao.
Funzo
Hakuna mtu anayeweza kuziba nafasi ya mama katika mioyo yetu

0 comments: