heeeeeeeee kumbe watu ndio wako hivi????? Duh

17:28:00 Unknown 0 Comments



Mambo ya ajabu ajabu usiyoyajua kuhusu binadamu

Wakati wewe unatoa mimba, kuna mtu anasaka mimba kwa miaka kumi na zaidi bila mafanikio

Wakati wewe kijana una mkataa binti uliyempa mimba, kuna mzee ana miaka nenda rudi akiwa anakesha akiomba Mungu amjalie mtoto

Wakati wewe una inyanyasa familia yako leo, kumbuka kuna mtu anatamani apewe familia na aipende

Wakati wewe unaichukia kazi uliyonayo, kuna mtu ana vyeti vyake safi ila hajawahi kupata kazi ya aina yoyoye na anaishia kwenye interview tuu

Wakati wewe unaichukia nyumba unayoishi sasa, kuna watu hawana sehemu ya kulala usiku wa leo

wakati wewe unakula na klusaza chakula na kumwaga kuna mtu leo hana uhakika wa kula


Wakati binadamu wengine wanafurahia kuua kuna watu wanahangaika kuhakikisha wanajaribu kuokoa maisha ya ndugu zao bila mafanikio

Wakati wewe humshukuru Mungu kwa uhai ulionao, kuna mtu ni mwaka wa nne sasa naumwa na yupo kitandani hajui ni lini atatoka ndani mwake akiwa mzima

Wakati wewe unawadharau na kuwasahau wazazi wako bila kuwajali. Kuna watu wanalia usiku kucha na kuumia kuwakosa wazazi

Wakati wewe ni bingwa wa kupoteza marafiki kwa ubinafsi wako kuna watu walia pamoja na fedha na mali walizonazo ila hawana marafiki wa kukaa nao na kuwashauri

Kumbuka, hakuna maisha yoyote zaidi ya haya na huna budi kuwa na shukrani kwa kile unachojaliwa sasa....

Pia ni bora kuwa na mpangilio wa maisha ukimtanguliza MUNGU na
kushukuru kila ulichonacho na kufurahia nyakati ulizonazo


Soma maoni ya wadau kwa kubofya HAPA

You Might Also Like

0 comments: