Valetine inanipeleka kaburini.....Naumia kumwacha mwanangu kwani naye atanifuata
Ilikuwa ni miezi sita imepita kabla ya kuumizwa vibaya na kipenzi cha roho yangu Suphian.
Sikuwahi amini kuwa suphiani angekuwa hivyo pamoja na kupewa maneno ya umbea juu ya tabia yake ya kuchanganya lakini inibidi niamini hasa kwa mkasa uliotokea.
Valentine day ya mwaka juzi nikiwa nimelala zangu nyumbani, suphiani alikuja akiwa na marafiki zake na kunichukua mpaka nyumbani kwake na kushangazwa na maandalizi yaliyowekwa pale.
Alinunua mbuzi mzima,vinywaji vya aina tofauti na kualika marafiki zake na tukafurahia sana siku ile akityita sio wapendwa wake hasa hasa mimi na mwishowe kuamua kwenda disco kuimalizia siku hiyo.
Mtoto nilijiweka sawa sawa na kuamini nina kila sababu ya kusifiwa na suphian huku nikiwapa taabu vidume wenye uchu wa kuparamia kila wakionacho bila kujali kinamilikiwa na serikali kuu au serikazi za mitaa.
Disco lilikuwa tamu na kila mtu alichanganyikiwa kwa furaha mpaka pale niliposhtushwa na kibao cha uso na kuona nuru yote imenipotea na giza likitanda kabla ya ngumi ya sikio iliyonifanya nisisikie chochote zaidi ya sauti za nzi waliosikika masikioni mwangu.
Sikujua kilichoendelea ila nakumbuka asubuhi niliamka nikiwa hospitali ya mkoa na mwili ukiwa kama umewekwa makaa ya moto kwa maumivu yake.
Baada ya kusimuliwa niliambiwa kumbe suphian akikuwa kaoa na mkewe kamtelekeza huko morogoro.
Na siku hiyo mke alikuwepo pale mjini akijaribu kufuatilia nyendo zetu na kujionea yale mahaba yetu kuanzia nyumbani na sasa akaja disco akiwa na kikosi cha wahuni ili kumsubu anayeibia utamu wake.
Akatushambulia ingawa suphian alikimbia kwa kutoroshwa na mwenzake na kuniacha mie nikidhalilishwa kwa kuchaniwa nguo na kipigo huku wakinibaka hadharani wale wanaume na mie nikiwa sijitambui kwa pombe na kwa maumivu ya kipigo pia.
Nililia kwa zaidi ya miezi nikimlaumu suphian kwa kunidanganya kuwa hana mke na kwa mpango wa kunivalisha ile pete ya uchumba siku ile.
Nikaapa kuwa kamwe nisingeweza kuja kumpenda au kumwamini mwanaume yeyote yule duniani.
Miezi minne kabla ya valentine ya mwaka jana nikampata kaka mmoja ambaye yeye hakuwa mpenzi lakini kila siku nikajikuta nikivutiwa na ucheshi wake Uelewa wake, kujali kwake na mara kwa mara nikawa nikitoka nae kwenda out kama rafiki na kufurahi sana.
Sikumbuki ilikuaje lakini huyu sasa aliniteka hasa baada ya kunitambulisha kwa mama yake na dada zake na baadhi ya watu wake wa karibu na kueleza mpango wa kunichumbia tena
Sisi wanawake tuna tatizo moja Fuledi, ni wepesi wa kumwamini mtu bila kuwa na data zake na pia twasahau kwa urahisi maswahibu yetu katika maisha.
Basi akaniambia baada ya valentine angependa kunivisha pete ya uchumba na kuwa hapendi iwe siku ya valentine kwani itanitonesha na kuyaamsha maumivu yangu ya mwaka jana.
Wow!! Kwangu lilikuwa ni neno la faraja na mapenzi ya dhati kutoka kwa mwanaume anayetambua umuhimu wa binti na anayejua kukumbuka maumivu ya moyo ambayo mpenzi wake kapitia na hapendi kumkumbusha.
Nilikubaliana nae kwa sauti moja na mabusu moto moto na kimwambia hisia zangu kwake na kuwa sasa nimepata mfariji wa matatizo na mtu wa kunipa mwongozo wa nini cha kufanya ili nami nimpende vile atakavyo.
Siku ya valentine nakumbuka nilivaa vazi langu nililonunuliwa nae mwezi mmoja uliopita lilikuwa ni zuri na likiashiria na kuonyesha maana rasmi ya neno wapendanao.
Mimi nilikutana nae mchana muda wa lunch alipokuja kazini kwangu na kuniletea kadi, ua na keki nzuri ya siku hiyo akionyesha kunijali mpaka marafiki wakanionea gere.
Jioni tukakubaliana kwenda kwenye hotel moja maarufu kwa chakula cha jioni tukiwa wawili tu ili tujadiliane.
Maongezi yalipamba moto na baadae meza yetu ikaandaliwa na kuwekwa mvinyo na chakula nasi kwa mahaba na raha zetu tukaanza kulishana kabla ya binti mmoja kuja bila kuongea na kuanza kujibizana na mpenzi wangu.
Nilipoingilia ugomvi nilijuta kuzaliwa kwani walinivamia na kunichana na nyembe usoni na kunifanya kuwa na kilema kwani mpaka sasa sina jicho moja kutokana nyembe kunichanja jichoni na baadhi ya maeneo ya uso wangu.
Ukweli ni kwamba yule dada amezaa na yule kaka na wakaona kwa harusi na binti aliurudishwa kwao kutokana na shari za mawifi na akatelekezwa huko na mumewe bila ya kupewa matumizi.
Cha kusikitisha zaidi ni kuwa kumbe alimwambukiza na UKIMWI bila wote kujua mpaka mke yule magonjwa yatokanayo na msongamano wa mawazo yalivyoanza kumwandama na yeye kuamua kupima na kujikuta ni mwathirika.
Naumia kwani kwangu kila VALENTINE DAY imegeuka na kuwa moto na kunipa kumbukumbu mbaya sana kama wengi watakavyoishia kuyakuta kesho na wengine walivyo na experience nayo....
Hivi sasa nimeshajiandikisha katika kituo cha kupatiwa ushauri nasaa na nina mtoto mdogo niliyemzaa mizezi saba baada ya lile tukio.
Dada na wadogo zangu,
Mnatumiaje nafasi ya siku hii katika kuchunguza mahusiano yenu na kujiweka sawa?
Hapa ni vyema kuyajua yafuatayo
1. Kutolewa out siku ya valentine sio sababu ya kutanua miguu yako kwa kila mwanaume, kwani kutakuwa na Valentine nyingi zijazo katika maisha yako hivyo chagua mwenza sahihi na kujipa muda nae.
2. Valentine sio siku ya ngono au kutafuta machumba ila inaweza kukupa mwanga na muda wa kujifunza zaidi maana ya neno wapendanao
3. Vakentine sio siku ya kujaza nafasi katika hotel na nyumb za kulala wageni bali siku ya waoendao hawa katika mahusiano ya kimapenzi kukaa na kuongelea kwa undani hatma za mahusiano yao.
4. Sio kila valentine day ni siku ya kuwaonyesha watu mpenzi mpya uliyenaye
5. KWA WANAUME: Ni vyema nanyi sasa kuwaonea huruma hawa na kuwa na misimamo ya kimapenzi kwa kuwa na binti mmoja ama kuwa wakweli zaidi.....
Kwa upande wangu kila valentine nitazidi kulia na kujutia yaliyonifanya kuwa hivi mapaka naingia kaburini.... Eeeh Mung nipe moyo wa amani na uvumilivu
Asanteni
Kama unamjali pia VALENTINE WAKO. Comment herufi yake ya kwanza na mpe neno zuri
Nawatakieni VD njema

0 comments: