BADO HUJACHELEWA KUYABADILI MAISHA YAKO

14:00:00 Unknown 0 Comments



Kama unakula vyakula ovyo ovyo, anza sasa kula vyema.
Kama unataka kupunguza uzito, anza sasa kufanya mazoezi.
Kama wewe ni mbinafsi, acha sasa kuwa mbinafsi.
Kama unamsaliti mpenzi wako, acha sasa hiyo tabia.
Kama unahitaji kubadilisha kitu katika nyumba yako, badilisha sasa.
Kama moyo wako unampenda mtu Fulani, nenda sasa na mwambie hisia zako 
Kama unataka sasa kuanza kumpa nafasi ya kwanza Mungu katika maisha yako, fanya sasa.
Kama njia uendayo sasa katika maisha yako ni mbaya, badilisha na kuifuata njia njema.

Wewe pekee ndio unayefahamu njia sahihi ya kubadilisha maisha yako.

Bado haujachelewa kuyabadili maisha yako na kuanza na njia mpya na njema kwako.

Kama Mungu amekulinda na umzima mpaka unasoma ujumbe huu, basi unakila sababu ya kushukuru na kuanza kuweka maisha yako kuwa mazuri zaidi na yenye mafanikio kwa njia halali.

Bado hujachelewa badilika sasa 

You Might Also Like

0 comments: