Simu ya android kidogo iniue kwa presha
Adroid!!! Adroid!!! Adroid!!! Adroid!!! Adroid!!!, simu za Android zilinifanya nikawa mtumwa na kamwe sikutaka kuona naishi bila kuzimiliki.
Na kwa kuwa sikuwa na fedha za kuweza kununua hata zile za hali ya chini basi nilijitahidi kuazima kwa wenzangu pale nyumbani au hata kusubiri watoke kazini nami niweze ingia FB, Whatsapp na Instagram.
Kipindi hicho ndio kwanza nilikuwa nimehitimu masomo yangu katika chuo fulani cha utalii hivyo nikawa na hamu ya kupata kazi na kujiwekea kuwa mshahara wangu wa kwanza utakuwa ni wa kununulia simu ya android.
Mungu hujibu sala zetu hatimaye nikafanikiwa kupata kazi na mwisho wa mwezi ulipofika nikampigia jamaa yangu mmoja kuwa nahitaji anisaidie tutafute simu hiyo ili muda huo huo ikiwezekana ninaze harakati za mtandaoni.
Jamaa akasema tukutane katika bar moja maarufu hapa mbeya na baada ya kufika tukaagiza chakula, wakati huo mie hata chakula hakipandi nawaza juu ya kupata simu.
Akanitoa wasiwasi na kusema niache mambo ya kwenda dukani kwani bar hiyo kuna vijana hupitisha simu za android na wao huuza kwa bei rahisi sana nusu au hata robo ya ile ya dukani.
Nikakubaliana na kuanza kupata moja moto na bari punde akaja kijana mmoja na kutuonyesha simu mmoja ambayo kwa dukani nafikiri ingefikia bei ya laki sita au zaidi na akawa anataka kiuza kwa laki mbili na nusu tu.
Tukamshusha mpaka akakubali kutuuzia kwa bei ya shilingi laki na nusu nami nikawa nimesevu hela nyingi hapo na kuipeleka kaunta ianze kupata chaji na kisha mawasiliano yakaanza..
Niliitumia ile simu na kila mtu alikoma kwani mwembwe hazikwisha kila mtandao wa kijamii nipo na kila saa simu iko busy kwa kujibu sms na post za wadau na comments zao pia.
Jana mchana baada ya miezi kama miwili kupita kuna jamaa kaja mpaka home na kuniuliza mimi ndio Daudi? nikajibu ndio akaomba aone simu yangu nikampa haraka nikijua atakuwa kapata habari kuwa namiliki simu ya maana.
Jamaa akaichukua na kuiweka mfukoni na kunipiga ngumi zaidi ya saba mfululizo na kisha kuwapigia jamaa zake wakanichukua mpaka kituo cha polisi na kusema tumemshika yule mwizi wetu ambaye tulichukua rb ya kumshika baada ya kutuibia simu nne , laptop 2 na fedha taslimu milioni nne na kuvunja kioo cha gari kwenye maegesho.
Jasho likaaanza kunitoka nikawa najitetea pale huku nalia na kuambiwa kama siwezi kulipa kesi iende mahakamani.
Nikalia kwa uchungu na kumwangukia jamaa yule magotini ili nimwombe msamaha kabla ya kushtuka naanguka toka kwenye kochi nililolilalia hapa sebuleni kwangu mchana huu.
Nimecheki simu yangu ipo najiuliza imekuaje niote ndoto hii wakati mimi simu zangu nanunua dukani?????
Bado sijapata jibu jama kanifahamuje au ndio hizi GPRS au Phone tracker au kuna nini?
Soma zaidi kwa kubofya hapa
0 comments: