Gauni la send-off lamfanya binti ahame mtaa..... mabinit wa dot kom changamoto

09:50:00 Unknown 0 Comments



Dada mmoja ambaye alikuwa anajiandaa kwa send off ya mdogo wake huku fedha za kununulia gauni la sare hana, aliamua kwenda duka moja kukopa gauni zuri kwa ajili ya kulivaa siku ya send off kama sare .

Baada ya send off akawa anadaiwa sana fedha ya lile gauni kiasi cha kukosa raha na ikafikia kipindi akaamua kubadili mpaka njia ili kukwepa kudaiwa ingawa bado mwenye duka alitumia kila njia hata ile ya kumfuata nyumbani kwake nyakati za usiku au asubuhi akiwa amelala au bado hajaamka.

Habari zikamfikia mama wa binti yule ambaye naye aliumizwa sana na mwanae kukosa furaha na alifahamu fika kuwa alifanya vile ili afurahie tukio la mdogo wake.

Hivyo mama huyo mfugaji wa kuku wa mayai akamwita mwanae nyumbani kwake na kumwambia mwanangu hapa sina fedha ila ninakupa trei 10 mayai ambazo ukiuza utapata zaidi ya elfu 60,000 na utumie fedha hizo kulipa deni lako na uwe huru.

Dada alifurahi sana na kumshukuru mama kwa upendo ule kwake na kuzifunga trei zile na kisha akaondoka ili akaziweke nyumbani na kutafuta mteja na hatimaye amalizane na deni lile.

Akiwa njiani akawa anawaza jinsi atakavyomlipa ile hela kwa dharau yule mwenye duka na akimpa pia atamwonesha kuwa yeye ni zaidi ya mbabe na hataki upuuzi wowote ule.

Akiwa ndani ya dimwi la mawazo yale kwa furaha akapiga makofi na kusahau kuwa alibeba trei za mayai nazo zikaanguka na halikupona hata yai moja na deni likaendelea pamoja na zile kelele.

Funzo

*Usiusherehekee ushindi kabla haujawa mikononi mwako
*Na katika kila jambo acha kujipa wakati mgumu wa kufikiri mpaka unasahau una dhamana gani umeishikilia kwa wakati huo
* Visasi au mpango wa kulipa jambo baya kwa baya mara nyingi huja na maumivu yake kwetu

Share comment comment yako
 HAPA


You Might Also Like

0 comments: