Haya sasa mimi nayaita majanga zaidi ya DENGUE
Palikuwepo mke na mume ambao walipendana sana, ila hawakuwa na mtoto hatimae wakaamua kumfuga paka kama mwana wao.
Baadae mke alishika mimba wakapata mtoto, walifurahi na kumlea kwa upendo wote.
Siku moja wakiwa wanapunga hewa bustanin mtoto walimuacha ndani kalala, ghafla walimwona paka wao akija amelowa damu akiwa na kipande cha nyama mdomoni.
Bila kuchelewa mke alishika gongo na kumpiga yule paka kichwani hatimaye paka alipoteza maisha papo hapo.
Walipoingia ndani walimkuta mtoto akiwa amelala kama walivyomwacha, na pemben mwa kitanda palikuwepo JOKA kubwa alieuawa na yule paka...
Mama alilia bila kupata jawabu hasa akijutia kitendo alichomfanyia paka wake na baada ya kugundua kumbe damu zile zilitokana na jitihada za kumwokoa mwanae.
Ebu nipe jibu umejifunza nini kutokana na habari hii?
Usiombe ukutane na wanamziki wakiwa wanachukua video zao na wakusimulie mikasa yao..
Hebu tazama mkasa huu
0 comments: