Hotuba bora na yenye kuumiza ya bwana harusi akishukuru kamati na wahudhuriaji

17:12:00 Unknown 0 Comments




MC: Na sasa tupate maneno machache kutoka kwa bwana Harusi

BWANAHARUSI: Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu. Pili nimshukuru baba mwenye nyumba wangu kwa kukubali niwe na deni la kodi ili kufanikisha harusi hii.

 Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii. Naishukuru kamati yangu ya harusi kwa kuwezesha kukusanya fedha zilizofanikisha harusi hii, nimshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana.

 Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama jirani kwa kuja na vyakula toka makwao ili kufanikisha harusi hii, na vijana kwa kuja na pombe za halali na haramu mradi harusi hii ni furaha tupu. 

MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali tulipane kidogokidogo aksante sanaaaaa

Soma maoni ya wadau HAPA

You Might Also Like

0 comments: