Soma jinsi jamaa alivyofanikiwa kutoroka jaribio la kuchunwa ngozi

17:21:00 Unknown 0 Comments



watatu walikamatwa na wachuna ngozi. Wakaambiwa kuwa watauliwa kisha watachunwa ngozi na ngozi zitaenda kuuzwa Nigeria. Wale wachuna ngozi wakawaambia kila mmoja anapewa nafasi ya kuomba jambo moja tu la kufanya kama kuomba dua au kuandika wosia.

Jamaa wakwanza akasema ye aomba auliwe haraka haraka sasa hivi bila maumivu makali. Wale majinamizi wakakubali ombi lake na kumpulizia nusu kaputi kisha wakamchoma sindano ya sumu. Jamaa wa pili akaomba karatasi na kalamu aandike salamu zake za mwisho kwa familia yake, naye ombi lake likakubaliwa. 

Jamaa wa tatu akauliza “kwani ngozi zetu zinatumika kufanyia nini?” wale wachuna ngozi wakasema “zinatengenezewa ngoma za kuleta utajiri” yule jamaa akatikisa kichwa kumaanisha ameelewa kisha akaomba kiwembe kikali, wale wachuna ngozi wakashangaa kwa nini anaomba kiwembe badala ya kuomba kitu muhimu kwa wakati kama huu, hata hivyo wakampa kama walivyoahidi. 

Yule jamaa akachukua wembe na kuanza kujichana chana mwili mzima huku akipiga kelele “x#@z sana nyie yaani ngozi yangu mnataka muiwambie ngoma, tuone sasa naitoboa yote kama mtapata mteja”

Soma wadau HAPA

You Might Also Like

0 comments: