Huyu Jamaa mzima kweli?
Nilikua naenda Kahama (Shinyanga) kikazi. Asbh mapema sna niko ubungo nikapata tiketi ya dirishani. Muda kidogo akaja Jamaa akakaa pembeni yangu nikajua niko nae siti moja. Sasa mshangao ndo uliponianza:
Safari imeanza jamaa kaweka begi lake akatoa maji makubwa na keki mbili akala. Sikushangaa. Kufika Chalinze kanunua Mayai ya kuchemsha 3 na Hindi 1 la kuchemsha na Soda ya kopo (Fanta) akapiga taratiiibu!! Tumefika Msamvu!! Kashuka karudi na Chipsi Mayai kanikuta nimekaa kwenye siti maana sikushuka. Gari halijaondoka kaita muuza korosho kanunua pakti kubwa huku kachukua machungwa 4. Mimi nikaanza kua na mashaka nae aisee!! Jamaa kapiga Taratibu!!
Tumeingia Dodoma saa saba hivi Heee!! Pale Four Ways watu tunashuka mchana tukafinye maana njaa sasa ilikua inauma Jamaa nae kashuka nikaguna MHH!!! Lahaula!! Jamaa kaingia Hotelini nae kaagiza Wali Samaki na Coca cola. Kwa kweli mimi nikaanza kumuogopa yule Jamaa!!! Nikaanza kufikiria mbona haombi kuchimba dawa?
Muda umefika gari linaondoka nikajua Jamaa lazima ataomba kuchimba dawa!! Lazima akakate GOGO!! Mhh!! Jamaa kainuka kavuta begi lake kapekua pekua karudisha kukaa namuona kashika Pande la muogo wa kuchoma mfuko wa karanga mbichi na maji ya Kilimanjaro makubwa!! Kwenye mfuko wa shati kuna biskuti za chokleti. Nikainuka mbio mpaka kwa Dereva. Niliogopa AISEE!! Nikasema "HIVI HUYU AKIJAMBA HUMU NDANI ITAKUAJE?"
Hivi huyu alikua mgonjwa au? Maana niliamua kushuka nikabadili gari!! Watu wengine HATARI!! Anaweza kutengeza BOMU tumboni!! Hahahaaaa!!!
0 comments: