Jamaa amweka mke rehani

08:48:00 Unknown 0 Comments

Waifu wa jamaa mmoja alikuwa akisumbuliwa sana na njemba fulani iliyokuwa ikimtaka kila
siku, hatimae waif akamwambia mumewe.

Mume akamwambia mkewe, "Unajua watu kama hawa dawa yao ndogo tu,we mkubali tu, ila
mwambie aje mlale hapa kwetu, mi ntajificha uvunguni na panga.

Akisha ingia ukiona kamaliza
kuvua nguo we ning’iniza mkono anza kuuchezesha, mi nikiuona ntatoka uvunguni na kumfunza adabu".

Mamaa akafuata masharti ya mumewe na.hatimae akaweza kuirubuni njemba hadi wakaingia chumbani, mume akawa tayari na
panga uvunguni mwa kitanda anangojea signo.

Jamaa alipovua shati, mke alishangaa kuona njemba ina makovu makubwa kifuani na
mgongoni akaamua kuuliza, "Hee jamani mbona una makovu hivyo?",

Njemba huku ikiendelea kuvua suruali ikajibu," Niwe mkweli mie nina pepo la kupenda wake za watu, waume wengi wamekuwa wakipanga kunifumania,
nimeshafumaniwa mara kumi na tisa, na wote walionifumania nimewaua".

Mamaa akbaki kuduwaa tu. Jamaa alipomaliza kuvua nguo
mdada akaanza kuning’iniza mkono ili mumewe atoke uvunguni, mume kabana kimya, kila jitihada za mdada kupunga mkono hazikupata majibu, mpaka njemba ikamaliza shughuli zake
akatokomea.

Ndipo mume akatoka uvunguni
jasho linamtoka,"Sasa ndio umefanya nini mume wangu? Umeacha nimeshindwa kufanya lolote, kwanini hukutoka jamanii?" .
Mume akajibu kwa ukali," We we we, mwenyewe umesikia kasha ua
19 unataka niwe wa ishirini? nauliza unataka niwe wa 20 kusudi muendelee na uasherati wenu?"

You Might Also Like

0 comments: