Kijana afanikiwa kuwasha gari lisilo na injini

05:02:00 Unknown 0 Comments



Kijana aliyedhihakiwa jeshini kwasababu ya imani yake alitumwa na mkuu wake apaki gari vizuri, akajibu kuwa hawezi kuendesha gari.

Mkuu wake akamjibu kwa dharau "mwombe Mungu wako akufundishe!" 

Kijana akaingia garini, akamwomba Mungu akawasha gari na kulipaki vizuri kabisa.

Alipogeuka akakuta mkuu wake pamoja na wote waliokuwa naye wameanguka kifudifudi huku wakimwomba Mungu..

Katika tahamaki mkuu akamwambia "Mungu wako ni mtukufu sana mwanangu, hilo gari halina injini lakini kwa maombi umeliwasha!"

Kama ukitazama vizuri utagundua kuwa kuna mahali uliwahi ulipitia na ni nguvu za Mungu ndizo zilikuvusha bila ya msaada mwingine.

Na pia kuna mahali ulishindwa kuitetea imani yako kwa kuogopa kuchekwa na watu au usahaulifu ulikaa kimya na kukosa kufikia malengo au kushinda mitihani ya kidunia.

Leo hii mwambie neno moja la kumshukuru Mwenyezi Mungu...... soma maoni ya marafiki hapa

You Might Also Like

0 comments: