Kwa kisa hiki nafikia kusema wanawake ni zaidi ya wauaji
Miaka kadhaa iliyopita nikiwa kidato cha sita nilibahatika kukutana na binti mmoja aitwaye Fatma ambaye yeye alikuwa akisoma shule jirani na alikuwa naye kidato cha sita pia.
Mungu mkubwa wote tukafanikiwa kufaulu na wote tukajiunga na elimu ya juu, mimi nikawa SUA na yeye akawa pale UDSM ila akawa anakaa kwenye hostel moja jina kapuni.
Tukawa na mazoea ya kutembeleana karibia kila weekend na yeye alikuja Moro na mimi nikawa naenda hostel kwake na kweli alifahamika sana SUA kwa baadhi ya marafiki na mimi pia Hostel yao hasa chumba chake walinifahamu sana kwani kuna kipindi nilikuwa nikilala weekend nzima kama mfuko hauko safi.
Siku moja niliamua kwenda kwa kushtukiza pale na baada ya kufika nikagonga mlango bila kufunguliwa na nikiwa nimekaa pale alikuja room-mate wake na kusema Fatma ameondoka na yupo mjini kujinunulia mahitaji.kwa kuwa sikuwa na issue yoyote na nimechoka na safari nikaamua kukaa pale pembeni ya mlango kwani kulikuwa na viti.
Rafiki yake alinisihi tuondoke pale lakini kwa kuwa nilikuwa nimechoka niligoma na kila nikijaribu kumpigia Fatma simu ilikuwa imezimwa.Hivyo na rafiki akakaa pale na hakugusia kunikaribisha ndani.
Kumbe muda wote huo Fatma alikuwa mle ndani akiwa na jibaba moja bila ya mimi kujua.Baada ya mimi kuanza kuhisi kuna ka mchezo nikaamua kuganda pale na rafiki wakaja na kila walipotaka kunitoa machale yakazidi kunipanda.
Sikuamini muda mchache baadae nikaanza kusikia minong'ono ndani la kile chumba na nilipokuwa nikiendelea kusimama pale sauti ya Fatma ikaanza kuita mwizi mwizi. Ilikuwa ni kitendo cha dakika chache tuu watu walijaa na nikiwa sijui nini chaendelea mara nilianza kupigwa na watu.
Walinipiga kwa muda mpaka alipofika jamaa mmoja na kusema mbona mnaye mpiga kama huwa na muona hapa, watu wakaacha kumpiga na kunikuliza mimi ni nani.Nikawasimulia kuhusu mimi na Fatma na kuwa ilikuwa ni njia ya kunitimua pale. Na jamaa kuanza kutoa kipigo kwa Fatma na yule mzee.
Basi nikatoka na kuanza kutafuta sehemu ya kulala usiku ule na asubuhi yake kuanza kurudi Moro huku nikiwa sina jibu sahihi ya nini cha kumfanya Fatma zaidi ya kusema kamwe usimwamini mwanamke aliyeko mbali na wewe na zaidi akiwa chuo
Soma mwendelezo wake HAPA
0 comments: