LEO RAFIKI YANGU AMEOKOA MAISHA YANGU
Marafiki wawili walikuwa wanatembea jangwani, mara wakaanza kugombana na mmoja akamchapa mwenzake kofi, yule aliyechapwa kofi akaskia uchungu lakini hakusema kitu, akaandika juu ya mchanga,"LEO RAFIKI YANGU AMENICHAPA KOFI..
Wakaendelea na safari yao wakafika kwenye dimbwi la maji wakaamuwa kuogelea, mara yule aliechapwa kofi akaanza kuzama, na Rafiki yake akamwokoa, alipopata nafuu akaandika juu ya jiwe,
"LEO RAFIKI YANGU AMEOKOA MAISHA YANGU.
Yule rafiki aliemchapa mwenzake kisha akamwokoa akamuuliza "Kwanini baada ya kukuchapa kofi na kukuumiza uliandika juu ya mchanga, na sasa nimekuokoa ukaandika juu ya jiwe??
Rafiki yake akatabasamu akamwambia "Rafiki yako anapokukosea unafaa kuandika juu ya mchanga, na ndipo upepo wa msamaha utafuta kile ulichoandika, na Rafiki yako akikufanyia jambo lolote zuri, tunafaa tuliandike kwenye jiwe la kumbukumbu ya moyo, pahali ambapo hata upepo hauwezi kufuta..
Kumbuka KUANDIKA JUU YA MCHANGA kila baya kutoka kwa rafiki yako na kulitunza lile zuri...
like Tabasamu na Fuledi
0 comments: