Mke amuumbua mmewe kanisani mbele ya waumini
Kulikuwa na familia moja ya wacha Mungu vizuri
tu pale Dar es salaam. Walikuwa wakisali kanisa
moja la kilokole.
Mwanaume alikuwa na tabia ya
kulala usingizi kila akiingia kanisani kusali. Siku
moja mke wake akagundua dawa ya kumfanya
jamaa aache kabisa tabia hiyo mbaya ya kulala
kanisani.
Unajua ni dawa gani hiyo?
Kukiwa tu ndo ibada imeanza, jamaa alianza
kuuchapa na mke bila kukawia alimminya kwa
haraka akamwambia,
“Mchungaji amekuteua ufunge ibada kwa
maombi”
Mwanaume akasimama haraka na kuanza
kushusha maombi makali ya kufunga ibada
“Baba katika jina la Yesu tunakushukuru kwa
ibada nzuri, na ya miujiza. Tunaomba ututangulie
tunapokwenda majumbani kwetu kupumzika,AMEN"
Baada ya kumaliza ibada, alijikuta kanisa nzima
likimkodolea macho huku wengine wakicheka
sana, na wengine wakiwa midomo wazi na
wengine wakiinama kwa aibu kwani ibada ndo tu
ilikuwa imeanza na jamaa anashusha sala ya
kufunga ibada! hii kali.
Nimesikia kuwa huyo bwana aliacha hiyo tabia ya
kulala lakini sikujua mahusiano yake na mke wake
yaliendelea kuwa mazuri au la.
0 comments: