Naomba kama kuna mtu humu ndani ni mtaalamu wa sayansi ya kale anipe ushauri.

19:30:00 Unknown 0 Comments

Hello Fuledi,

Naomba kama kuna mtu humu ndani ni mtaalamu wa sayansi ya kale anipe ushauri.

Ni wiki ya pili sasa tangu nifumaniwe na mke wa mtu, cha ajabu yule jamaa pamoja na kuwa nasikia ni baunsa sana lakini hakunipiga wala kusema lolote zaidi ya kuninyofoa kanywele kamoja sehemu zangu za siri na kuondoka nako.

Nimevumilia lakini naona nazidi kukonda kwa mawazo na nimejaribu kupeleka baadhi ya wazee wenye busara wakaongee nae lakini anadai hana shida yoyote na wala hajamfukuza wala kumpiga mke wake.

Jamani nisaidieni maana hali yangu inazidi kuwa ya kudhohofika kwani sili na sipati usingizi.

Je nini anaweza kuwa anapania kukifanya kwangu??

You Might Also Like

0 comments: