Siku nilipoamka nakujikuta nipo mochwari
Nilikuwa mtumwa wa pombe mpaka kuna wakati nikahisi labda kuna mchawi anafanya hivyo na kwa jinsi livyozidisha nikaja kuamini kuwa sasa huyo mchawi wangu kafariki kabisa.
Kila siku ilikuwa
ugomvi sio tuu ule wa mimi na familia bali hata ule kati ya mimi na wale
nitakaokutana nao huko bar na ni mara chache sana niliweza kuamka asubuhi
nikiwa sina makovu ya kipigo cha jana yake.
Mbaya zaidi kuna siku
nilitoka kwenye pombe na kuanza kuendesha gari kwenda ueleko usio wa nyumbani
na mbaya zaidi ni pale nilipofika sehemu nikazidiwa na kupaki gari pembeni
nikiwa nimejifungia na kama sio baadhi ya wasamaria kuvunja kioo basi ningefia
mle ndani kwa kukosa hewa.
Ile hali ikaanza kuwachukiza
wanangu na familia yangu kwa ujumla pamoja na mke wangu ambaye yeye alishaongea
na kuamua kukaa kimya. Na mimi nikaona sasa kama spidi ndio inazidi pamoja na
kupewa aina mbalimbali za dawa na sala za kuacha pombe.
Siku moja mida ya saa
kumi na moja baada ya kufanya kazi nikaamua kupitia bar moja na kuanza kupata
vinywaji.. Kwa upande wa kazi kila mtu alinipenda ila ikifika suala la pombe
kila mwana familia alinikimbia.
Basi mimi nikapiga
pombe pla e na nakumbuka mara ya mwisho tulikutana na jamaa yangu ambaye
tukaanza kuzipakia vilivyo kabla ya kuachana mida ya saa sita naa usiku ambapo
kumbukumbu zikakata kabisa.
Kaubari ka saa kumbi
na mwili na kelele za watu zikanifanya nishtuke na kujikuta nipo kwenye chumba
nisichokifahau ila pembeni yangu kulikuwa na mtu aliyelala nikawa namwamsha
mama mary!!!!!! mama mary amka!!!!!! bila kushtuka.
Nikaamka ili niwashe
taa na kwenda uani kujisaidia mara nikaona nimekanyaga mtu ila nae hashtuki
kabala ya taa kuwashwa na mlinzi kutoka mbio huku akipiga kelele maiti!!!!!
imeamka maiti imeamka...........!!!
Nilipogeuka na
kuangalia vyema nikagundua kuwa nipo mochwari na nilishawekwa namba mguuni na
kuvalishwa yale mashuka yao.. Nilitoka mbio nikikimbia huku kila aliyeniona
akitimka kabla ya kuiona boda boda ambayo kila nilivyomkimbilia alizidi
kuongeza mwendo kwa uoga.
Wazo likanijia
nikaingia nyumba moja ambayo nao baada ya kelele nikawaelewesha na nikaomba
wanipe msaada nguo na kasha kurudi nyumbani ambako nako kila mtu alikuwa
akinisubiri na wakisema kuwa walinitafuta usiku kucha bila kujua wapi nipo.
Siku msimulia mtu
yoyote juu ya ule mksasa na kuanzia hapo pombe niliiacha na kila nikiiona pombe
natamani kukimbia…. Ila juzi nimejua ukweli kuwa ule mpango ulisukwa na wanangu
wakishirikiana na mama na badhi ya marafiki lakini bado nimejikausha.
Pombe ikizidi sana
itakuwa sooo
Hadithi hii haina
ukweli wowote ni njaa za mchana zinafanya niwe mpuuzi
soma comments za wadau HAPA
0 comments: