Ungekuwa wewe muuzaji ungefanyaje?

21:42:00 Unknown 2 Comments


Mwanadada mmoja alienda super market kununua kuku, bahati mbaya kwenye friji kulikuwa na kuku mmoja tu...muuzaji akamtoa akamuweka kwenye mizani, akaonekana ana kilo moja na robo.

Mdada akamuuliza muuzaji, "Huna mkubwa zaidi?"

Muuzaji akamchukua yule kuku na kujifanya kamrudisha kwenye friji, halafu akamtoa tena kwenye friji na kumrudisha kwenye mizani, safari hii akagandamiza mizani kwa gumba... kuku akaonekana ana kilo mbili.

Mwanadada akasema, "Duh afadhali huyu mkubwa kidogo, naomba unifungie nawachukua wote wawili."

Ungekuwa wewe muuzaji ungefanyaje?

You Might Also Like

2 comments:

  1. Ha ha ha unatumia busara kumuelimisha kuwa huyu mkubwa ana order sasa kama wachukua sawa ila wa kilo 1.5 atachukuwa mwenye order

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha ha ha hapo mtihani

    ReplyDelete