Vitu vya msingi kuzingatia katika maisha yako
1. Kuwa karibu na wazazi wako na familia yako pia
2. Kuwa makini na kila kitu katika maisha yako
3. Kuwa na kiu ya kuipenda afya yako,kufanya kazi kwa bidii, kula na kuvaaa vyema
4. Usijihusishe na mambo yasiyo na faida katika maisha yako
5. Jali thamani yako machoni mwa watu hata kama unapitia katika nyakati ngumu maishani mwako.
6. Usiuabudu umbea
7. Kuwa makini na marafiki unaowachagua kuwa nao maishani
8. Usicheze na muda kwa kuamini kesho ipo
9. Kuwa halisi wakati wa kupanga plan zako na hakikisha kila mara unazipitia kuona kama uko sahihi
10. Kuwa mwerevu kwa kuishi vyema na jamii inayokuzunguka
11. Andaa mipango inayoendana na wakati uliopo.
12. Maliza kazi zako kwa muda muafaka
13. Usilale kwa kuchelewa ukijitetea kuwa unamalizia kazi, panga muda wako kwa kufanya kila jambo kwa wakati wake
14. Hakikisha unatatua kwa busara, hekima na uvumilivu mkubwa kila tatizo linalokukabili katika maisha yako
15. Usiwe mtu wa lawama kila mara kwa wakuzungukao
16. Jitahidi kuwa mtu wa kuyakubali makosa yako na sio kumrushia mwenzako
17. Heshimu kila anayekuzunguka pamoja na changamoto zao
0 comments: