Kuna mambo napenda tuongee kidogo hapa.
Hata kama hautakomenti ila najua utakuwa umesoma tu na kiburi kitakufanya upepese macho.
Kila mtu anaruhusa ya kupenda kile apendacho bila ya kubughudhiwa na mtu yoyote yule.
lakini jamani kuna watu wananiboa kidogo na hawa nitawaweka katika makudi na kuwaelezea kama wafuatavyo:
1. Wavutaji sigara
2. Walevi
3. Mashabiki wa mpira
4. Walokole
Wavutaji sigara wao saa nyingine wanakuwa feki kweli, mtu mpo katikati ya mazungumzo bila hata kufikiri kuwa mliopo pale sio watumiaji wa bidhaa hiyo basi ataiwasha na kuanza kuwafukiza mimoshi kwa staili tofauti mara autolee puani mara pua moja mara sijui nini bila kujua wengine mnakerekaje na moshi huo.
Kama haitoshi ataanza kukuongelesha kakusogezea mdomo jumulisha na shida ya ya mjini kuwa na miswaki ya asili yenye kuondoa uvundo basi manweza mkaamua kumaliza kikao hata kabla ya muda.
Ndugu zangu hawa walevi wao wana mengi sana maana wewe umetoka ukae sehemu angalau japo nawe utulize maumivu ya wiki kwa kupata moja moto moja baridi kama yeye, usiombe akufahamu na kalewa hata kama kuna kikao nyeti utaamua uhame eneo mara hiki mara kile mara nataka bia.... ni kero yaani unajiuliza huyu jamaa katoka kwake mbalizi kuja town kuomba bia au ni asili yao kuwa wasumbufu?
Mashabiki wa mpira, kumbukeni sio wote tunaopenda mpira wengine tunakuja kusindikiza marafiki zetu na kuamua kujitenga na kuendelea na mazungumzo yetu... Sasa shida ni pale timu ishinde au isishinde amani huwa haipo nyakati zote kuna watu wana midadi ya kukupasua na ngumi au hata ukajikuta meza yako imeangukia miguuni.... wazee mtusaidie na sie tuwe na faragha sio wewe unakuja meza hawakujui na kuanza kusimlia mpiraaa weeeeeee huku unanipotezea windo na muda kumrudisha mtu sijamwaga neno
Walokole, Hawa ndugu ukiposti kitu hapa FB wao wanakuja direct inbox ndugu sijui nini na nini mara hiki na kile kama wewe unaona u rafiki yangu na post au chochote ninachokiandika kiko tofauti na mila au imani yako........Mlango uko wazi au tulia ili nami niitumie akaunti yangu kwa malengo yangu....
Samahani lakini ni mtazamo wangu..... haya hayapo kwenye katiba ni yangu tuu
0 comments: