Barua ya Segito kwenda kwa MUNGU

13:22:00 Unknown 0 Comments



Siku moja mfanyakazi wa Posta akiwa katika kazi yake ya kupanga barua alikuta barua moja imeandikwa "Kwenda kwa Mwenyezi Mungu". Akashangaa lakini kwa udadisi akaamua kuifungua. 

Ilikuwa imeandikwa:

"Ee Mungu, mimi ni mwanamke mjane, kikongwe wa miaka 85. Jana wakati natoka hospitalini
niliibiwa pochi yangu ambayo ndani yake ilikuwa na akiba yangu ya muda mrefu sana ya shilingi laki 1.
Kama unavyojua nilikuwa na mpango wa kuwaalika kina bibi na wazee wenzangu kwa sherehe ya kutimiza miaka 85. 


Hapa nilipo sijui nitafanya nini. Mimi nimemua kukuachia wewe kila jambo kwa sababu sina tena tumaini. Watoto
sina, wajukuu sina, shida tupu, sina anayenijali na kibaka naye umemwacha hadi akaniibia. Nimeona
tu niandike kukueleza jinsi gani moyo wangu umeumia. Nisamehe kama nimekosa. Naomba msaada
wako.


 Ni mimi mja wako, 

Segito."
Jamaa aliyekuwa anaisoma akaguswa sana moyoni, akawakusanya wafanyakazi wenzake wakachanga hela ikafika 96,000 wakaituma kwa yule bibi siku ile ile. Wakawa wana furaha kwamba wamefanya jambo jema. Siku
zikapita na baada ya mwezi jamaa akaona tena barua toka kwa yule yule bibi ikiwa imeandikwa "Kwenda kwa Mwenyezi Mungu".


Akawakusanya wafanyakazi wenzake wote akaifungua wakaanza kuisoma.
"Ee Mungu, 

sijui nikushukuru vipi kwa maajabu uliyonitendea. Nilifanya sherehe nzuri na wazee wenzangu na nashukuru kwa  kuniwezesha kufurahia siku hizi za mwisho katika uzee wangu huu na nimetoa ushuhuda kwa marafiki zangu juu ya matendo yako makuu. 

Hata hivyo hela ilikasoro shilingi 4,000. Nadhani wizi huo ni kazi ya wafanyakazi wa Posta maana ni wezi, walafi na wasio na huruma hata kidogo.,

 Ni mimi mja wako

 Segito."

You Might Also Like

0 comments: