Club imeniweka pabaya sasa nawindwa na watoa roho ( kisa cha kusisimua)
Nilishapanga kuwa lazima ijumaa ile nihakikishe naenda disco hasa ukizingatia nilisikia kuwa vyuo vimefungua na wanafunzi wamewekewa boom nikajua kwanja litanoga sana nami nikipata chance ya kuibuka na totoz.
Niliwahi sana kurudi nyumbani kutoka kazini kwani sikupitia sehemu yoyote ile zaidi ya kuongoza kwangu kisha nikaoga na kuuweka mwili saafi na kuwasha gari kutafuta sehemu nipate chaula kwani mida ilikuwa tayari imesonga sana.
Saa mbili na nusu nilikuwa nishamalizana na kula na sasa nipo sehemu napata bia nikisubiri mida ya saa nne na nusu niingie club na kupata mziki mwanana huku nikikodolea mimacho totoz.
Nikiwa pale nakunywa kuna binti nilimwona kwa mbali kakaa kwenye meza moja pee yake huku akiwa busy na kitu mkononi anachezea nikajua itakuwa ni simu na sikumwangalia sana nikaendelea na mambo yangu ingawa sura ikawa akilini mwangu.
Ulipita muda nikiwa pale na nikaona kuwa sasa wakati ulikuwa unaniruhusu kwenda club, hivyo nikawasha gari na kuanza safari.
Nilifika pale na kuchukua tiketi yangu na nilivyoangalia mbele yangu nikaona yule binti niliyemwona pale bar nikiwa nakunywa yuko pale pia ... sikutaka kuhoji amefikaje ila nilichofanya ikawa ni kuingia ndani.
Mziki uliendelea nami nikakaa kwanza pale kaunta na kunywa zangu bia ambapo dakika chache baadae yule dada akaja pale na kuanza kunywa wine yake jambo lililonifanya nianze utaratibu wa kujisogeza kwake kwa kuongea naye kidogo.
Kila dakika nilivyoongea nae pamoja na kuonekana anakunywa wine yenye kilevi kikubwa na kwanywa chupa kadhaa lakini bado macho yake yalionesha kuwa makavu na mwenye aibu pia. Nikajihoji au yeye akilewa anakuwa na aibu au aibu za nini?.
Nikajua kuwa huyu mtoto atakuwa mwaka wa kwanza na kaingia chuo bado ni mwoga mwoga wa kuwepo mazingira kama hayo lakini lile la macho kuwa makavu wala hapepesi ikawa tatizo.
Baada ya pombe kunikaa nikaanza kucheza nae huku nikipumzika na kwenda kaunta kukaa kisha nacheza naye tena...,lakini maajabu ni kwamba nikiwa nacheza naye naona kama ana mguu mmoja na nikirudi kukaa kaunta nikimtizama vizuri naona ana miguu miwili basi nikahisi labda ni mimi pombe zinanikolea.
Nikacheza naye na kumwacha pale ndani kisha nikawasha gari kwenda zangu nyumbani nikapumzike ili siku ya pili niwahi kazini mapema. Nikiwa njiani taa inamulika nikamwona yule binti akinisimamisha kutaka lifti na kashika viatu mkononi.
Nikasimama na kumuuliza kuna nini? Akaniambia alipanda bodaboda ila mwenye bodaboda kumbe ni kibaka kamwibia pochi yake na fedha zake na kumwacha pale.
Mida hiyo ilikuwa tayari ni saa tisa ya usiku, nikamuuliza sasa si nilikuacha pale umefikaje huku? Akanijibu nilivyokuwa mimi nageuza gari yeye akaona hana wa kucheza naye na amechoka akachukua bodaboda na kuwahi kuondoka.
Nikaondoka naye moja kwa moja mpaka nyumbani kwangu na kumshauri alale pale ili asubuhi aende kwake. Kwa kuwa nilikuwa na chumba kimoja cha kulala pamoja na sebule tuu nikaona yeye alale chumbani nami sebuleni.
Akalikataa wazo hili na kusema kwani nikilala naye nitaweza kumdhuru? Nikasema hapana, akasema wala usijali mimi nakuona kama vile wewe ni gentlemen so sina hofu na wewe.
Nikaenda kulala lakini muda huo pombe zilikuwa nyingi kichwani na nikaona uvivu kwenda tena mpaka sebuleni kuzima taa hivyo nikaona nimwombe anizimie taa.... Nilishikwa na butwaaa kwani hakuamka ila mkono ulirefuka mpaka kwenye switch .... nilipiga kelele na sauti haikutoka nikatoka mbio mpaka nyumba ya jirani.
Nikagonga mlango kwa fujo sana pale mpaka ukafunguliwa, ile unafunguliwa naona ni yule binti ndio anaufungua, nilirudi mbio uelekeo wa nyumbani kwangu, wakati huo kuna gari lilikuwa linakuja mbele yangu huku najaribu kulisimamisha mpaka kulisogelea barabarani lakini halikusimama. Nikabaki nikawa nimechnagnyikiwa na nikiwa sijui nini cha kufanya nikaanguka pale chini kwa kuishiwa nguvu.
Nikajivuta taratibu kwa kujiburuza mpaka karibu na kwangu kabla ya fahamu kunitoka na saa kumi na mbili kasoro baba mmoja nyumba ya jirani akaja na kunichukua baada ya kuniamsha sana na kisha kuniuliza kwanini nimelala pale nje ya nyumba?
Nikamwambia kuna mambo yamenitokea jana yake lakini sikutaka kumpa story yote.
Nikakimbia na kwenda kwa kwa rafiki yangu wa damu Suphian na kumsimulia kisa hata kabla sijamaliza akaniambia binti wa aina hiyo alimfuata jana yake usiku na kumwambia aje kuniambia kuwa sasa kazi ndio imeanza na lazima nikome.
Jasho likaanza kunitoka nisijue nini cha kufanya ingawa suphian akaniambia nihamie pale yaani nisirudi nyumbani na tutakuwa wote mpaka liishe kisha tukajiandaa na kisha kwenda kazini.
Tukiwa kwenye gari tunashuka nje ya ofisi wote kwa pamoja tukamwona yule yule binti akiwa mbele yetu tena na nguo zilezile alizozivaa jana na akaingia ofisini kwetu.
Tukakimbia mpaka ofisni tukamuuliza secretary kama kuna mtu amemwona akiingia akasema hapana, ile tunaendelea kubishana pale na suphian kuwa yule ndio yule binti naye bakisema ni kweli sasa kaelekea wapi??? Mara ghafla namwona...................................................................
Ili kumalizia kisa hiki comment neno "MALIZIA" na kisha tuma 1500 kwa njia ya tigopesa/airtell money nami nitakutumia inbox
0713317171/0684868191 kumbuka kunitumia na jina lako la facebook
Soma hapa <<<<<<< MAONI >>>>>>>
0 comments: