KABLA YA KUACHANA NA MPENZI WAKO WA SASA NA KUJIPELEKA HUKO UENDAKO, TAFADHALI SOMA RASIMU HII

21:13:00 Unknown 0 Comments



1. Jipe nafasi ya kutosha kutafakari kama ni kweli sasa hana maana tena hata kama amekukera

2. Chunguza kwa makini kama kuna hali inayomfanya kuwa hivyo na jaribu kumsaidia aitatue na awe kama mwanzo

3. Orodhesha kila baya na jema na ona upande upi umezidi na hata mmoja ukielemewa angalia
wewe umechangia upande upi katika hayo.

4. Kumbuka mahusiano ya kimapenzi sio sawa na
mchezo wa ngonjera ambao una wimbo wa kuingilia na wa kutokea. Usitoke na wimbo wa mbwembwe nyingi za kumponda halafu baada
ya kuumizwa huko uliko ukaanza kuutafuta wimbo wa kumrudia

5. Mapenzi ni kupitia changamoto na vikwazo mbalimbali mkiwa pamoja na kisha kuyatatua
kwa pamoja.

6. Shetani unayemjua ni bora kuliko malaika usiyemjua. Hapa kumbuka hakuna mahusiano
yasiyo na matatizo yake hivyo vumilia ulipo.

7. Mapenzi ya mwazo huwa na kila aina ya furaha ingawa ni wachache wanaoweza kubakia na hali hiyo hivyo kuwa na msimamo hapo
ulipo

8. Kama unahitaji furaha na mahaba ya dhati anza kwa kutengeneza hapo ulipo usije
tegemea kuwa kuna mtu atakupa furaha kabla ya wewe
kuitengeneza furaha hiyo.

9. Ushawishi wa zawadi na fedha sio mapenzi kwani hata changudoa siku hizi wanatoa zawadi
za pipi ukiwachukua lakini wao wanatengeneza mazingira ya kukukamua hela vyema hivyo
ikubali hali yako.

10. Hakuna hali inayodumu, kama
unamkimbia kwa kuwa ni maskini au ana maswahiba yake binafsi kumbuka hayo ni mapito na baada ya kila usiku mchana nao huja na mambo mapya.

La ziada, kama ukiona umeshindwa haya yote
basi wewe rudia kusoma tena na tena na kuongeza yako mpaka mrudiane na ikishindikana wewe soma tuu

Ila unaweza share

You Might Also Like

0 comments: