Kama una kaka, mme, dada, au mtu yoyote ambaye unamtafutia dawa ya kuacha POMBE ...Jaribu hii ni rahisi
Nilikuwa mtumwa wa pombe mpaka kuna wakati nikahisi labda kuna mchawi anafanya hivyo na kwa jinsi livyozidisha nikaja kuamini kuwa sasa huyo mchawi wangu kafariki kabisa.
Kila siku ilikuwa ugomvi sio tuu ule wa mimi na familia bali hata ule kati ya mimi na wale nitakaokutana nao huko bar na ni mara chache sana niliweza kuamka asubuhi nikiwa sina makovu ya kipigo cha jana yake.
Mbaya zaidi kuna siku nilitoka kwenye pombe na kuanza kuendesha gari kwenda ueleko usio wa nyumbani na mbaya zaidi ni pale nilipofika sehemu nikazidiwa na kupaki gari pembeni nikiwa nimejifungia na kama sio baadhi ya wasamaria kuvunja kioo basi ningefia mle ndani kwa kukosa hewa.
Ile hali ikaanza kuwachukiza wanangu na familia yangu kwa ujumla pamoja na mke wangu ambaye yeye alishaongea na kuamua kukaa kimya. Na mimi nikaona sasa kama spidi ndio inazidi pamoja na kupewa aina mbalimbali za dawa na sala za kuacha pombe.
Siku moja mida ya saa kumi na moja baada ya kufanya kazi nikaamua kupitia bar moja na kuanza kupata vinywaji.. Kwa upande wa kazi kila mtu alinipenda ila ikifika suala la pombe kila mwana familia alinikimbia.
Basi mimi nikapiga pombe pla e na nakumbuka mara ya mwisho tulikutana na jamaa yangu ambaye tukaanza kuzipakia vilivyo kabla ya kuachana mida ya saa sita naa usiku ambapo kumbukumbu zikakata kabisa.
Kaubari ka saa kumbi na mwili na kelele za watu zikanifanya nishtuke na kujikuta nipo kwenye chumba nisichokifahau ila pembeni yangu kulikuwa na mtu aliyelala nikawa namwamsha mama mary!!!!!! mama mary amka!!!!!! bila kushtuka.
Nikaamka ili niwashe taa na kwenda uani kujisaidia mara nikaona nimekanyaga mtu ila nae hashtuki kabala ya taa kuwashwa na mlinzi kutoka mbio huku akipiga kelele maiti!!!!! imeamka maiti imeamka...........!!!
Nilipogeuka na kuangalia vyema nikagundua kuwa nipo mochwari na nilishawekwa namba mguuni na kuvalishwa yale mashuka yao.. Nilitoka mbio nikikimbia huku kila aliyeniona akitimka kabla ya kuiona boda boda ambayo kila nilivyomkimbilia alizidi kuongeza mwendo kwa uoga.
Wazo likanijia nikaingia nyumba moja ambayo nao baada ya kelele nikawaelewesha na nikaomba wanipe msaada nguo na kasha kurudi nyumbani ambako nako kila mtu alikuwa akinisubiri na wakisema kuwa walinitafuta usiku kucha bila kujua wapi nipo.
Siku msimulia mtu yoyote juu ya ule mksasa na kuanzia hapo pombe niliiacha na kila nikiiona pombe natamani kukimbia…. Ila juzi nimejua ukweli kuwa ule mpango ulisukwa na wanangu wakishirikiana na mama na badhi ya marafiki lakini bado nimejikausha.
Pombe ikizidi sana itakuwa sooo
Hadithi hii haina ukweli wowote ni njaa za mchana zinafanya niwe mpuuzi
Umetisha
ReplyDeleteasante
ReplyDelete