Majeruhi wa ajali ya ndege asimulia alivyosota kwenye kisiwa cha ajabu kisicho na watu kwa miezi kadhaa
Rubani mmoja wa ndege alipata majanga akiwa angani baada ya ndege yake kuanza kushika moto, yeye pamoja na abiria wake wakawa hawana jinsi zaidi kutumia parachitu ili waweze
kujiokoa.
Parachuti ile ilimpeleka rubani yule baharini na baada ya siku nzima ya kuogelea kwa bahati nzuri rubani yule akiwa peke yake alijikuta katika kakisiwa kadogo ambako watu hawaishi huko .
Maajabu ya kisiwa kile kilikuwa na kabonde kadogo alikoweza kupata maji ya baridi (yasiyo na chumvi).
Rubani Yule ilimbidi atumie majani ya minazi mitano aliyoikuta pale ili aweze tengeneza sehemu ya kujisitiri usiku pamoja na kuwasha moto (kwa njia ya kupekecha) atakao utumia kuchomea samaki ili ale pamoja na kujilinda dhidi ya viumbe hatari waishio majini.
Kwa uzoefu wake wa miaka mingi katika masuala ya anga na baharini alijua kuwa eneo lile kamwe asingeweza kupata msaada wowote kwani hakuna meli wala boti ambayo ingeweza kufika pale na pia
kwa kuwa kale kakisiwa kako katikati ya bahari ni dhairi eneo lile hakuna meli ambayo ingeweza tia nanga hivyo meli na boti hupita kando ya kisiwa
kile tena mbali sana.
Rubani yule aliishi pale kwa zaidi ya wiki bila ya mafanikio na kuanza kujiona kama mtu
aliyetupwa kwenye dunia yake isiyokuwa na msada wa aina yoyote ile. Kazi yake kubwa ilikuwa ni kuvua samaki, na kuja kuwachoma na kwa kuwa kuni zilikuwa zaenda kuishia hivyo alijitahidi kuufumbika moto na kuutumia usiku tu.
Rubani yulealiishi pale kwa zaidi ya wiki bila ya mafanikio na kuanza kujiona kama mtu
aliyetupwa kwenye dunia yake isiyokuwa na msada wa aina yoyote ile. Kazi yake kubwa ilikuwa ni kuvua samaki, na kuja kuwachoma na kwa kuwa kuni zilikuwa zaenda kuishia hivyo alijitahidi kuufumbika moto na kuutumia usiku tu.
Siku moja akiwa bondeni anajitafutia samaki na maji ya kunywa ghafla akahisi kama kuna harufu ya moshi ikambidi arudi kwenye kiota chake mara moja.Kufika pale akashangaa kuona upepo ulipuliza ulemotona kuunguza kuni zake na kibanda chake kwa hiyo hata weza kula wala kuwa na moto tena.
Kwa uchungu mwingi rubani Yule alijitupa chini na kulia huku akiwaza kuwa sasa Maisha yatakuwaje bila ya chakula, moto na hata kula samaki wa kuchoma tena?
Baada ya kuwaza na kulia kwa muda mrefu akapitiwa na usingizi mzito na kulala zaidi
ya masaa matano.
Baada ya kuamka akiwa na uchovu na njaa akashangaa kuona kwa mbali kuna meli inakuja na baada ya kukaribia ikatia nanga wakashuka watu na na baada ya kuwauliza walijuaje kuna mtu pale jamaa wakasema tukiwa kwa mbali tuliona kuna moshi unafuka hapa tukajua kuwa kuna watu wanaishi hapa hivyo tukaamua tuje tutafute maji ya kunywa kwani tuliishiwa kwenye meli yetu.
Baada ya hapo jamaa akapata lifti na kurudi kwao
Funzo
· Kila jambo katika maisha yetu hutokea kwa sababu maalumu na mwisho wa siku lazima jibu
litokee.
· Mungu wetu ni mwema na hujibu maombi kwa muda muafaka na wala hachelewi
comment na share kama umenielewa
0 comments: