MATUMIZI YAKO YA SIMU NI SALAMA ?
Bwana Juma ni Dereva Taxi maeneo ya Mwanyamala kwa kopa siku moja alifuatwa na jamaa mmoja ampeleke sinza kwenye nyumba Fulani ya wageni.
Walipofika pale Yule jamaa akasema ameishiwa chaji kwenye simu yake akamuomba juma simu yake atumie kupiga ili awasiliane na mwenyeji wake pale nyumba ya wageni , simu ya juma haikuwa na hela .
Walipokaribia ile nyumba ya wageni Yule jamaa akaomba kushuka anunue vocha atie kwenye simu ya juma halafu awasiliane na mwenyeji wake , juma akakubali , jamaa akanunua vocha akaingiza kwenye simu ya juma halafu akawasiliana na mwenyeji wake .
Walipofika sehemu husika jamaa akashuka akaingia ndani ya nyumba kumfata mwenyeji wake ambaye alikuwa mwanamke huku juma akiwa ameshaondoka zake kwa sababu alikuwa ameshakamilisha shuguli yake .
Siku iliyofuata iligundulika maiti ya mwanamke ndani ya kile chumba , simu ilikuwa mezani na vitu vingine vyote hakukuonyesha kama kulikuwa na vurugu au mikiki yoyote ile.
Uchunguzi wa awali ulifanyika pale chumbani kwenye kifaa cha kuwekea taka na simu ya Yule mwanamke , hapo mwili wake ulikuwa chumba cha maiti ukifanyiwa uchunguzi pia .
Kwenye kifaa cha kuwekea taka iligundulika vocha moja iliyotumika , ilipofuatiliwa iligundulika iliwekwa kwenye simu ya juma ikatumiwa kumpigia huyu mwanamke aliyekutwa na mauti
.
Dereva wa taxi akatafutwa akapatikana , kukaguliwa gari yale ikagundulika vocha nyingine ya simu iliyotumika katika moja ya milango ya taxi hiyo .
Bwana Juma yuko Ndani kwa mashtaka ya mauaji na uchunguzi unaendelea kufanyika mpaka hapo itakapokuja kujiridhisha si yeye aliyefanya tukio hilo .
Inawezekana wewe ukawa ni bwana juma ajaye , unayependa kugawa simu yako tu kwa watu wapige , watu waingize vocha zao , watu waandike ujumbe mfupi au wafanyie chochote kile bila kujua unachofanya kinaweza kuhatarisha maisha ya wengine na yako pia .
Simu na namba yake ni mali yako imesajiliwa kwa jina lako , wakati unasajili uliingia mkataba wa kutumia kifaa hicho bila kuvunja sheria zozote za nchi muda wote.
Kina juma wako wengi , tazama usiwe mmoja wao .
Chanzo: Kutoka kwa rafiki
0 comments: