Mfanyakazi adakwa na hirizi ofisni kwake jioni hii.....................AIBU SANA KWA VIJANA KUAMINI NDUMBA

23:36:00 Unknown 0 Comments



Email niliiona jumamosi majira ya saa moja na nusu asubuhi nikiambiwa kuwa natakiwa kuanza kazi jumatatu yake na pia natakiwa niwahi kwani kutakuwa na mafunzo ya awali ili kunijengea uwezo wa kuanza kuyamudu majukumu yangu ipasavyo.

Nikamkumbatia mke wangu na wote tukafurahi na hakika furaha ilikuwa kubwa hasa ukizingatia nilikaa nyumbani kwa muda bila kazi maalumu huku majukumu yakizidi kuwa makubwa na magumu kwa upande wangu kama baba wa familia asiye na kazi.

Jumatatu niliingia mapema pale kazini na kuanza mafunzao yaliyodumu kwa siku nne na baada ya hapo nikakabidhiwa ofisi yangu na kuwa sasa nitaanza kufanya kama meneja mkuu wa kampuni hiyo ya ununuzi huku tukijiandaa kwenda site mpya ya kazi.

Siku moja asubuhi baada ya kufungua ofisi, nilishangaa sana kuona kuna bundi kafia juu ya meza yangu. Nikatoka haraka na kumuuliza secretary wangu lakini nae akaonyesha hajui lolote.

Nikaona labda alifia tuu kwa bahati mbaya ila jioni ile wakati wa kurudi nyumbani nikaona ni vyema sasa niondoke na funguo zangu ili nisiweze hisi jambo baya kwa mtu maana huwezi jua hizi kazi za watu.

Siku nne baadae nikiwa nafungua ofisi nikakutana na kitu kama  kinyesi cha mtu mzima kikiwa juu ya kiti changu na mlango ulifungwa pamoja na madirisha yote na hakuna aliyekuwa na ufunguo zaidi yangu.

Nikaifunga haraka ofisi na kukimbia mpaka hoteli jirani na baada ya kukaa pale kwa dakika nikitafakari nikaanza kuhisi ya kuwa kuna jambo linakaribia kutokea na mawazo ya haraka yakaja kuwa nimfuate yule boss wangu ambaye ni mzungu nimwambie lakini nikaona ataniona sina elimu nawazia uchawi.

Nikarudi na kufuta kile kinyesi pale ofisi kwa siri ingawa muda huo nilishauliziwa na boss lakini secretary akawa amewaambia boss kuwa nilienda kupata chai mara moja.

Kazi zikaanza kuwa ngumu na mbaya zaidi kuna siku nilingia ofisini na baada ya kuufungua mlango nikakutana na nyoka aliyekufa akiwa chini sakafuni. Wakati huu niliamini kuwa secretary na mzee ambaye ni mfagizi wetu walikuwa wanahusika.

Nikarudi nyumbani na sikutaka kumsimulia mtu ila sassa nikaanza kuhisi mchezo huo utakuwa ni nmzito sana. 

Weekend nikaamua kwenda mpaka Mbozi kwa babu mmoja  na akanipa dawa na kunihakikishia kuwa kijana wangu Fred hapa hakuwezi mtu tena ni michezo ya watu ambao wanaitaka nafasi yako.

Zilipita siku mbili bila vimbwanga nikaona dawa ya mzee chikanga inafanya kazi na kama haitoshi sasa ndani ya siku hizo mbili nikawa niko busy na kazi za pale ofisini kabla ya siku ya tatu kuona kobe yuko juu ya kiti changu wakati nafungua ofisi.

Wakati huu nikaona inaweza kuwa sio ofisini mbona wafanyakazi wote wako safi na hakuna aliyekuwa akitaka ile nafasi??? Na hata secretary na yule mzee kamwe wasingefanya upuuzi huo.

 Nikakumbuka kipindi sina hela nilikuwa na mahusiano na binti mmoja na tukaachana vibaya akiniambia lazima nikome atanitafuta kila kona mpaka niumie zaidi yake..

Nikaamua kwenda kumwomba msamaha ingawa hakutaka kabisa kukubaliana au kunisamehe akidai ni lazima niende kumwomba mke wangu msamaha kwa kutoka nje ya ndoa ndio nae atanisamehe na sitaona tena mauzauza.

Nikawaza kuhusu hilo na kwenda kwa wife ingawa sikuwa na nguvu na ujasiri wa kuanza kumweleza lakini nilishangaa jinsi alivyonisamehe na kuniomba nitulie bila kujua kuwa yale mambo ya ofisini ndio yamenipelekea kuongea naye.

Huwezi amini jumatatu yake pamoja na kuomba msamaha lakini nafungua ofisi nikaona hirizi kubwa sana pale ofisni kwangu na nikiwa sijui nini cha kufanya mwili wangu kwa uoga ukaanza kupandisha joto na nikafunga ofisi na kuomba niende kutibiwa ambako hawakuniruhusu kurudi nyumbani au kuendesha gari kwa kuwa BP ilipanda sana hivyo nililazawa pale kwa siku tatu.


Baada ya kutoka hospitali nikafikiria kuacha kazi ingawa nikaona haitakuwa suluhu na uamuzi mzuri kwani niliihitaji ile kazi na wakati huo tayari nimekuwa jirani sana na yule secretary wangu na nikamshirikisha akaniambia kabla ya kuja mimi kuwa boss pale kuna mzee alitamani sana awe bosi labda atakuwa huyo ndio mhusika.

Nilipelekwa na rafiki yangu mmoja kwa mganga mmoja ambaye yeye alinipeleka kwenye mto mmoja na kunizamisha zaidi ya mara tatu na kuruka moto kisha akanilambisha kisu na akanihakikishia kuwa hakuna kipya ila siku ya kwanza ofisini nijitahidi nichelewe kutoka nitamwona mbaya wangu na kwenye begi langu kuna aina ya maji yaliyonuka kama kinyesi akanipa nizunguke nayo kwa siku nzima...

Nilirudi ofisini nikiwa safi na najiamini sana na siku hiyo nilingia ofisini na kupokelewa na mkurugenzi wangu yule mzungu na akaniambia mbona nakuwa kama bado sijayazoea mazingira? Nikawa najikakamua pale kuonyesha nipo safi lakini mfukoni natembea na ule ushuzi wa mganga huku nikihisi kila mmoja ni mchawi anataka nafasi yangu..

Jioni ile nilikaa mpaka saa mbili bila ya dalili ya kumwona huyo mbaya wangu na matokeo yake siku ya pili naingia ofisni nikakautana na jogoo kakatwa kichwa na ujumbe kuwa sasa kama siiachii ofisi nitaona maana najitia kiburi.

Nilifunga ofisi haraka na kwenda kwa Mkurugenzi huku jasho linanitoka na aliponiuliza kuna nini nikamwambia nimepata taarifa za msiba wa baba kijijini hivyo natakiwa kuondoka haraka sana.

Bosi akanipa ruhusa na kuniambia nitumie gari la ofisi na nikapewa fedha ya mafuta na kurudi ofisini ambako yule kuku na kichwa chake na yale maandishi nikayachukua na kuyafungia kwenye begi langu na kuwasha gari na kuondoka bila kuacha ufunguo kwa spidi kali iliyochanganyikana na jamba jamba..

Sikutaka hata kumpigia mke wangu nilinyoosha mpaka kijijini kwetu na kumsimulia babu yangu hali halisi naye bila kuchelewesha akasema mjukuu nafuu umekuja maana ungeweza kufa.... nikaachia ushuzi mzito na kunyanyuka pale nikiwa natetemeka.

Akanifanyia utaratibu wa kunipeleka kwa mganga mmoja ambako nilipewa dawa na kukaa huko kwa siku tatu na niliporudi siku ya nne mkononi nilikuwa na dawa ambayo niliambiwa niirushie chumba changu pale ofisini usiku wa saa mbili na mambo yatakuwa sawa.


Kwa kuwa niliambiwa niitupie mida ya usiku basi moja kwa moja nikaiweka tayari na asubuhi nikaelekea kazini baada ya kumshirikisha mke wangu wakati huu. 

Pale kazini kila mtu alinipa pole ya msiba nami nikaichukua kama ilivyo na baada ya hapo kazi zikaendelea nikiwa na matumaini kuwa siku hii mbaya wangu angepatikana..

Nilifanya kazi mpaka mida ya kufunga ofisi na baada ya kumaliza nikaondoka kwenda bar ya jirani nikipata moja moja ilinisubiri muda watu wote wametoka ofisini niende nikairushe ile dawa na kurudi zangu home.

Nilichungulia na kuona kila mtu kaondoka hata gari la boss lilishaondoka, nikanyanyuka na kwenda mpaka pale ofisni na nikafanikiwa kufungua mlango na mlinzi hakuwepo wakati huo.

Nilipowasha taa kidogo nizimie maana yule boss wangu mzungu alikuwepo mle ndani na akaniambia alijua ningerudi tuu mle ofisini maana alikuwa akinifuatilia na mbaya zaidi niliumia baada ya kunisimulia kuwa yeye ndio alikuwa akiweka vile vitu vyenye mfano wa kishirikina.

Nilipomhoji ni kwa nini? 

Aliniambia sehemu ambayo tunaenda kufanya kazi watu wanaamini sana ushirikina na wameajiri zaidi ya mameneja 4 ambao walishindwa kuhimili kutokana na vitisho vya wenyeji na kukimbia wakijua wangekufa.

Sasa aliamua anifanyie huo mchezo ili kunijengea ujasiri na ndio mafunzo ya awali aliyoniitia niwahi pale ofisini..........JASHO LILINITOKA MAANA NILISHATUMIA HELA NYINGI KWA AJILI YA SAFARI ZA KIGANGA KUMBE NI MCHEZO.

 Basi nikiarudi nyumbani na kumsimulia mke wangu ambaye alinicheka sana na kumshukuru yule mzungu kwani bila yeye nisingeweza kufichua  juu ya yule mchepuko wangu.

Mpaka sasa ninaendelea na kazi na pamoja na vitisho nipatavyo bado niko ngangari na tunapendana sana na mke wangu pamoja na wafanyakazi wenzangu.

Angalia wasemavyo marafiki HAPA




You Might Also Like

0 comments: