Mzee mwenye busara feki adakwa muda huu hapa jijini mbeya

21:20:00 Unknown 0 Comments




Mzee mmoja wa busara alisimama mbele ya kundi la watu wenye msongamano wa mawazo juu ya maisha yao na changamoto zake na waliokata tamaa na kuona maisha yamekuwa machungu kwako, Mzee akaanza kuwahutubia kwa kuwapa kichekesho.

Kichekesho kile kiliwafanya watu waangue vicheko kama vichaa wengine wakizidiwa na vicheko na kuanguka chini na wengine kutoa machozi kwa furaha isiyo na mfano.

Mzee akakirudia kile kicheko tena safari hii wakacheka wachache na wengine wakiwa wametulia na wachache wakionyesha kutabasamu tu.

Akakirudia tena kile kichekesho kwa mara ya tatu lakini wakati huu wakacheka wachache zaidi na wengi wakiwa wametulia na zile tabasamu hazipo tena usoni mwao.

Mara ya nne akakirudia tena ila wakati huu hakuna aliyecheka na kundi zima la watu walikuwa kimya wakimwangalia na hakuna hata tabasamu wala vicheko nyusoni mwao.

Mzee akatabasamu na kuwaambia, " Hamjaweza kucheka kichekesho kimoja kwa kila mara nilipokirudia, lakini kwa nini mnabaki mkilia kwa tatizo moja kila mara??''

Kamwe usifanye siku yako moja ambayo imekuwa mbaya ikufanye uone maisha yako yote yamekuwa mabaya.

Sio kisa eti leo imekupa maumivu basi na kesho haitakuwa nzuri kwako....

Napita

You Might Also Like

0 comments: