Siku wanandoa walipoamua wasiongee na wazazi wao......... Soma nini kiliendelea
Wanandoa wawili ambao walitoka kuoana, usiku wao wa kwanza baada ya harusi waliamua wakubaliane kulala na kutofungua mlango wao siku ya pili asubuhi hata kama nani angekuja kugonga mlango ili waamke.
Asubuhi yake wazazi wa kijana wa kiume wakaja na kugonga ule mlango bila mafanikio na kuamua kuondoka zao na wakati huo wote wale wanandoa walikuwa wanatazamana wakiwa kimya.
Mara wakaja wazazi wa binti nao wakagonga ule mlango lakini binti akiwa machozi yanamtoka akamwambia mme wake kuwa kwa kweli nimeshindwa kukaa kimya naomba niende kuwafungulia mlango kwani nimeshawakumbuka tayari na naona nashindwa.... Mme akamruhusu kwa roho safi.
Miaka mingi ikapita na wanandoa wale wakafanikiwa kuwa na watoto watano na wanne wa kwanza walikuwa wanaume na watano alikuwa binti pekee.
Wale watoto wakiume wote wakaoa na kwenda kuishi na familia zao na mtoto wa kike akawa bado anaendelea na masomo.
Ikafika muda wa yule mtoto wa kike kuolewa na baba yule akaandaa sherehe kubwa ya kumuaga binti yake kipenzi na kualika watu wengi na ikafana tofauti na zile za kaka zake na yle binti.
Watu wakamuuliza yule mzee, " kwanini umemfanyia sherehe nzuri huyu binti na kumpa zawadi nyingi na unafuraha kuliko kaka zake walipokuwa wakifanyiwa sherehe za kwenda kuoa?"
Yule mzee alijibu, " Nimemfanyia huyu hivi kwani huyu ndiye atakaye nifungulia mlango?"
Mzee huyu alijibu haya akikumbuka wakati wa harusi yake jinsi mkewe alivyoshindwa kuvumilia kutoufungua ule mlango.
Funzo
Kufungua mlango hapa ina maanisha kuwakumbuka wazazi hata baada ya kuoa au kuolewa
Watoto wa kiume huwa wagumu sana na wazito kuwakumbuka wazazi wao lakini wanawake zetu hutukumbusha sana.
Watoto wa kike ni zawadi, faraja, tegemeo, wasaidizi na ni waangalizi wa wazazi walio wengi hata baada ya kuolewa.
Pia wana upendo utokao moyoni mwao kama ule wa mama zao kwenye familia zao na ni wanyenyekevu sana katika majukumu yao tofauti na wanaume walio wengi
Ni kwa neno hili huwa napenda kuona marafiki zangu mkiandika kwa herufi kubwa "MUNGU MBARIKI MWANAMKE"
0 comments: