Unapopata bahati ya kuwa na mafanikio kamwe usiwadharau wakuzungukao...... Huyu yamemkuta
Mama mmoja alipata bahati ya kuolewa na mme mmoja ambaye alikuwa na utajiri mkubwa sana.Baba huyu alikuwa anafanya kazi katika taasisi moja ya kifedha katika nchi fulani na mkewe pia alikuwa mhasibu katika benki moja maarufu nchini huko.
Maisha yao yalikuwa gumzo mtaani kwani kila mtoto wao alisoma shule za nje ya nchi hiyo na pia kila waliporudi waliendesha magari tofauti ya kifahari na kutumia fedha kwa anasa.
Kila mwananchi wa mtaa huo alitamani maisha ya familia ile na kila mwisho wa mwaka familia ile ilitumia pesa nyingi kusafiri kwenda kijijini kusalimia wazazi huku kila mtu akiwa na gari lake kuanzia baba mpaka watoto
Mara nyingi yule mama alikuwa na dharau hasa akienda sokoni na buchani, alishangaa kuona mtu akinunua nyama nusu kilo badala ya mguu mzima wa ng'ombe au kisamvu ambacho yeye alidai kuwa ni mboga ya sungura.
Watu wengi walikereka na tabia ile na kumwambia ingawa yeye aliona ni sawa na alichukulia kama ni wivu dhidi ya utajiri wao.
Miaka kadhaa badae kuna wizi wa fedha ulitokea ofisini kwa baba na baba akasimamishwa kazi huku akipewa mshara nusu mpaka pale ushaidi ulipo kamilika na kuonekana kuwa alihusika na kuachishwa kazi bila kupewa haki zake.
Wakiwa sasa wanatafakari nini kinaendelea na wanatumia mshahara wa mke tu aliyebaki kazini na hawataki kuamini kuwa wanatakiwa kupunguza matumizi ya fedha mara mama naye akakumbwa na kashfa ya ubadhilifu wa fedha na kufukuzwa kazi na baadhi ya mali kama nyumba na maduka kutaifishwa na kubaki na nyumba moja waliyoijenga kwa siri maeneo fulani
Maisha yakawa magumu na wakawarudisha watoto kutoka masomoni nje ya nchi na kuwaleta nchini mwao katika shule za kawaida ingawa ilikuwa ngumu kwa watoto kuzoea mazingira haya kwank kwao ilikuwa ni kama kushuka thamani.
Mara wakaanza kusikia mtoto wao wa kike kawa changudoa ili apate fedha za matumizi kwa kuwa hadhi yake ilishuka kwa kukosa fedha kabla ya baba kupata mashtuko uliochangia kupooza mwili baada ya kusikia mtoto wao wa kiume naye kawa shoga ili aweze kupata fedha za matanuzi pia.
Miezi michache baadae baba akafariki na mama mpaka sasa anauza vitenge na nguo za kutembeza mtaani kama mmachinga na mpaka sasa watoto washaharibika.
Ndugu yangu nakusihi kamwe usidharau maisha na watu wakuzungukao kwani huwezi jua Mungu ana mpango gani na maisha yao na yako pia.
Mshukuru Mungu kwa kila baraka uliyonayo na kila mara mheshimu kila mtu na kuheshimu uwezo wake kifedha na hata mawazo kwani sote twamuomba baba mmoja ambaye ni Mungu wa watu wote na hutubariki tofauti kwa nyakati tofauti.
0 comments: