Vituko vya facebook kwa wale maskinii wa mawazo.

14:04:00 Unknown 0 Comments



1. Wengi wanapenda kuekti maisha ya kishua wakati wapo choka mbaya huku wakishua wenyewe wapo kawaida.

2. Wengi wanajifanya wamesoma st na intenational na waliosoma kweli wametulia wanaona kawaida.

3. Wengi wanapenda kupiga picha na magari ya kuazima, wale wamiliki wanapotezea wakijua ni lake hata wasipopiga nalo picha.

3. Wengi wanajifanya wanafanya kazi ofisi kubwa, wafanyakazi wa kweli wametulia hawajisifii wanakwepa mizinga.

4. Wengi wanapenda kupiga picha na nyumba kali hukuwa wamepanga, wenye nyumba kali wenyewe hawapigi wanahofia ujambazi.

5. Wengi wanapenda kuapload picha tuwajue ma hb au warembo, na ma hb na warembo wa kweli ni ngumu kuweka picha kukwepa usumbufu.

6. Wengi wanajifanya kwao kuna mabeki 3, wale wenye mabeki 3 kwao wapo kimya wanaheshimu thamani ya yule dada.

7. Wengi wanajifanya kwao kuna mkwanja mrefu, na mtu wale wenye mkwanja wapo kimya wanajua kitu cha kawaida.

You Might Also Like

0 comments: