Binti wa facebook ameyabadilisha maisha yangu... kanipa kazi, nyumba na usafiri...Naipenda facebook
Kwa kweli ilikuwa mara yangu ya kwanza kumshuhudia binti wa umri wangu akishuka katika gari zuri na la kifahari kama lile, na nikiwa nimezama kulishangaa gari ghafla nilianza kuona naishiwa nguvu hasa uzuri wake ulivyofanikiwa kunitoa jasho mchana ule.
Binti alikuja moja kwa moja mpaka meza niliyopo pale bar na kuuliza kama kuna mtu pale au angeweza kujoin meza ile.
Nikamjibu karibu na kuwa huru. Basi mie nikawa busy na ka HTC kangu nilikopata kama zawadi toka kwa besti yangu aliyeko masomoni huko china.
Binti akaagiza whisky moja matata na ya bei juu, mie nikaanza kuona hapa sasa majanga maana nikizidi kaa pale inaweza kuja round ya mimi mtu mzima nikaaibika hasa ukizingatia tarehe zile zilikuwa hazisomeki na meneja wetu mpya uso wa mbuzi huyo asingeweza hata kutoa Salary Advance… kwanza hebu tuachane na story za meneja wetu mpya maana naweza haribu sikuyangu.
Baada ya kuletewa kinywaji kile mimi nikajifanya kuomba bili yangu ili nisepe lakini binti akadai aaah mie nikaagiza yote hii nikijua nawe mtumiaji… karibu tujumuike.. Duh hapo pakawa pagumu kukataa nikaona soo maana sijaipiga ile makitu kwa muda sana…kwa haraka nikamwambia asante dada naingia maliwato mara moja kisha naja.
Baada ya kurudi tukaanza kushusha ile kinywaji na maneno yakisonga nikamwambia nipo mjini nimejishikiza sehemu ila hapalipi na yeye akaniambia anasimamia kampuni ya ujenzi ya baba yake na pia yeye ana kampuni ya matangazo.
Tukaendela na kazi ya kupiga vinywaji na siwezi kukumbuka nilifikaje nyumbani maana nilikuja kujikuta niko nyumbani na ni siku ya pili.
Zilipita wiki kadhaa bila kuwasilina nae kwani sikumbuki hata kama niliichukua namba yake ya simu, siku moja nikiwa facebook nachati kupitia ukurasa wa tabasamu na fuledi, nikaona picha ya gari kama la yule binti kwenye profile ya dada mmoja nikamuadd na baada ya kunikubalia nikakimbia moja kwa moja kwenye picha zake na nikafurahia kuona ni pic za yule dada bwana.
Nika mkumbusha nae akanikumbuka na alivyo mjanja akaenda kwenye post zangu na na kulike post moja niliyoiandika, “Noma sana hapa,bongo yaani kazi zote nzuri ni za wenye hela tu??? Ngoja nasi tusubiri bahati zetu” akaniuliza kwa nini nimeandika vile, nikampa ukweli jinsi kazi niliyonayo inavyoboa na ni tofauti na kile nilichokisomea yaani niafanya ili nisife njaa hapa mjini.
Wiki moja baadae akanipigia simuna kunialika ofisini kwake majira ya saa saba mchana,kufika pale nikakutana na baadhi ya watu wakiwa katika makao wa kumfanyia intavyu mutu, wakaniuliza maswali nikawa nawajibu na wakaniruhuru niondoke. Siku tatu baadae nikaitwa na kuambiwa wamenipa kazi na kuwa meneja uajiri katika lile kampuni.
Nilishindwa kujizuia kuachia kicheko cha furaha kwani sasa napewa nyumba gari na pia mshahara mnono na binti anaonyesha dalili za kunitaka niwe nnae.... duh yaani acha tu.
kwa furaha ya kazi mpya na hasira ya yule boss uchwara pale kazini kwangu, nikasema naenda kuandika barua ya kuacha kazi na kumpa yule mpuuuzi na meneja mjinga anayependa kutuonea wafanyakazi.
Baada yakufika job na kuwaambia wenzangu huku nikiwa nimeandika barua, nikakingia ofisini kwa boss nikampa barua akiwa anashangaa shanaa pale mimi kwa hasira nikasema najamba pale shuzi ndefu ili akome unoko wake.
Nikashtusha na kibao kutoka kwa rafiki yangu kumbe muda wote huu nikuwa nimelala ofisni baada ya kula…. Ama kweli ndoto za mchana mbaya sana
0 comments: