D' Banj adata baada ya kukutana na Bill Gates!

09:45:00 Unknown 0 Comments



Muziki ni kitu kinachoweza kukufanya kukutana au kubadilishana mawazo na watu usiowategemea,pengine ulikuwa unasoma habari zao au kuwaona kwenye televisheni tu na kufikiri kuja kuonana nao ni ndoto.. ndicho kilichotokea kwa D'banj aliyepata shavu la kuonana na kupiga picha na watu matajiri duniani.

Baada ya kuwasili Monaco tarehe 28 kwenye shughuli zake,alipata nafasi ya kusalimiana na kupiga picha na mmoja wa matajiri duniani Bill Gates. Pia alikutana na mmoja kati ya matajiri mashuhuri Africa mwenye asili ya Sudan Mo Ibrahim kitu kilichofanya ajivunie hayo mafanikio..

D banj na Bill Gates

You Might Also Like

0 comments: