DAh kuna marafiki wa blog hii wanazingua sana..Soma hii stori!!

21:57:00 Unknown 1 Comments

Asisee kumbe haka kablog ka tabasamu kanafuatiliwa na watu namna hii? Mie nilijua ni ka blog uchwara tuu duh we jamaa komaa unaweza kumshinda jamaa yule wa facebook.... Aliongea Dan kwa msisitizo

Mie nilishamzoea kwa matani yake na muda huu nilikuwa nimemweka chini kumpa mkasa ambao ulikuwa ukinikabili kwa kipindi hicho.

Wakati huo nilianza kutoa kwenye paseli na kuweka mezani waleti nne, pefume za bei kali kama sita dola elfumoja za kimarekani na simu nne aina ya HTC ambazo zilionekana kuwa ni brand new.

Kama haitoshi pia kulikuwa na badhi ya mashati ya kiasiki kutoka kwa wabunifu mavazi wa kibongo na mikufu ya maana.

Dan akaniukiza, umepata wapi vyote hivyo?

Sikuongea neno zaidi ya kumpa ka memo kalikoandikwa , " from your number one fan....... Fuledi your so hot... Mwaaa"

Umevipokeaje?

Nikamwabia, leo nimetoka posta na kufungua mail box ya tabasamu na nimeona hivyo sasa sijui huyu ni nani na kwa nini ananitumia hivi vitu.

Dan akaniambia " acha upuuzi Fuledi, huyu ni binti ambaye kakuzimia sana na atakuwa anafuatilia sana post zako na sasa ameamua akupe zawadi na atakuwa kakuzimia pia"

Nikamwambia sasa naweka post ya kuwakataza marafiki kunitumia zwadi bila kujitambulisha au kama vipi si wanipigie simu, kunitext whatsapp au hata kwa page?

Na pia mimi nimeoa so kupokea zawadi zenye majina ya you are hot sio mambo kabisa naweza sababisha ugomvi na mamaa kama akiwahi kwenda posta na kuona zawadi hizi.

Huku akishushia na funda la mwisho la bia yake Dan akasema kuna watu mafala sana, yaani unapata bahati mpaka mlangoni na unaiacha basi kama vipi nipe mie hizo zawadi.

Nikamgawia chache na nyingine kuwapa marafiki na kurudi nyumbani maana nilihofia kuwa na mavazi au manukato mapya nikabaki na fedha zile tu.

Ebwana kama nilifungulia zile zawadi zilizidi na kila mara nikapokea na kumpa rafiki yangu dan kwani hofu yangu kubwa ilikuwa kuvaa nguo au hata kula baadhi ya zawadi zake ila hela nikaziweka.

Hatukutumia namna nyingine ya mawasiliano zaidi ya posta aka SLP hivyo nikawa na uhakika wa kutodakwa kwani hata funguo za sanduku nilikuwa nazo mimi tu.

Rafiki yangu akawa anashangaa sana kwa jinsi nilivyopata bahati na hata kutamani iwe yake.

Ila muda huu kwa mbaaali nikajikuta naanza kuzipenda zawadi za HONEY JEI na mara kwa mara kuzipokea.

Muda ulipita na siku moja akaomba aje kutembea mkoa ninao ishi na mie nikamwambia Dan eeeh!!!! yule mtu wa zawadi anakuja sasa kwa kuwa mie nimeoa na naijali familia basi akija wewe jifanye ndio fuledi.

Dan akifurahia lile wazo na kuniambia nimakaribishe........

Honey Jei akatuambia kuwa atakuja kwa usafiri wa basi na kwa kuwa hapendi kuonekana kwa watu basi aambiwe eneo la hotel atakayofikia ilipo ili yeye aende na baade fuledi aende.

Kumbuka muda huo wote ilikuwa ni maeasiliano kwa box la barua na hapa mwishoni alitoa namba moja akadai haitakiwi kupigwa kwa sababu baba yake anamfuatilia sana hivyo ni sms tu.

Basi siku ya kuja ikafika na safari akaanza na wakati huu mrembo aka Honey Jei akawa yuko njiani akuwasiliana kwa meseji na Dan.

Mida ya saa moja jioni Dan akanipitia ili twende hotel mtoto alikofikia.

Tukafika pale na mie akaniacha bar nikipata kinywaji kama ninachokitumia muda huu na yeye kwenda chumbani ili ampokee mgeni na kisha aje naye tule chakula cha jioni kwa pamoja na kisha mie niwahi nyumbani.

Dakika mbili baadae hotel nzima ilikaa kimya baada ya sauti zilizoambatana na mbio kali zilizomfanya Dan kupitiliza mpaka kaunta na kisha kuzirai.

Bila kumuuliza Dan nini kimetokea haraka tukapanda mpaka uelekeo wa chumba na kugundua kuwa Honey Jei alikuwa ni mwanaume .........

Mpaka sasa kijana Dan amepona ila kapatwa na ugonjwa wa kushtuka shtuka kwani hata hii habari alivyoisoma alishia kushutuka na kama kushangaa kama wewe.

You Might Also Like

1 comment: