Jinsi nilivyoshindwa majaribio matatu ya kumwua kichanga wangu

20:18:00 Unknown 0 Comments


Binti mmoja mwenye miaka 25 miaka 30 iliyopita akiwa ndio kwanza kahitimu chuo na ndio anaanza kufikiri namna ya kuisaka ajira akajikuta akiwa na dalili za mimba, kwenda kupima ikaonyesha ule ujauzito ni wa miezi 4 na yeye akashangaa kwa nini hakuwa akihisi dalili hizo kwa muda mrefu.

Kwa kuwa alikuwa kakosana na mpenzi wake na wameshatawanyika kurudi makwao na wakati huo mawasiliano hayakuwa rahisi kama sasa na hata kama angefanikiwa alijua yangechukua muda kumfikia na jibu la mpenzi wange lingekuwa siitambui mimba hiyo.Binti akaamua kufa kisabuni na kunuia kuitoa mimba ile.

Alizunguka hospitali kadhaa na kwa madokta kadhaa lakini wote walionyesha kutokuwa na utayari kwani mbimba ile ilishakuwa kubwa na angeweza kufa yeye pamoja na mtoto wake au hata kupata madhara makubwa katika mfuko wake wa uzazi na kuja kuwa tatizo hapo baadae.

Ikapita miezi kadhaa na hatimaye yule binti akafanikiwa kujifungua mtoto wa kiume na kumwita Emmanuel bila kujua maana halisi ya lile jina kuwa ni "Mungu yupo pamoja nasi"

Binti akakaa na yule mtoto kwa miezi tisa na kuamua amtupe ili atafute kazi kwani alingeweza pata kazi akiwa na yule mtoto na pia hana mtu wa kumtunza yule mtoto. Pia akakumbuka wakati akiwa mjamzito jinsi alivyokuwa akikosa kazi kisa tumbo lake kuwa kubwa.

Binti akamchukua mtoto wake siku moja jioni na kwenda naye mpaka uchochoro mmoja na kuona sehemu ile kuwa hakuna mtu na kuamua kumweka pale na kuondoka, hatua chache mbele akashangaa kusikia sauti ya yule mtoto akicheka kwa furaha sana. Mama alishangaaa na kurudi pale kuona kuna nini, kufika pale akamwona mtoto akiwa na tabasamu zuri na yuko huru bila kulia wala nini. mama yule akaamua kumchukua mtoto na kurudi naye nyumbani.

Kufika nyumbani mama akasema atamweka kwenye maji na kumbana pua ili afe na ionyeshe kama aliangukia kwenye maji. Safari hii ile amemweka kwenye maji, mtoto alianza kuyafurahia maji tofauti na ilivyokawaida yake. mama akapatwa na hofu na kuhisi kuwa yule mtoto sio wa kawaida na kuahirisha mpango ule na kuendelea kumtunza.

Mtoto yule akazidi kuwa kwa kimo na maarifa na kisha kufanikiwa kusoma mpaka kumaliza digrii yake na hivi sasa ni mkurugenzi wa kampuni moja maarufu ya kusindika vyakula na amemsaidia mama yake katika umri wa miaka aliyonayo sasa 55 kuwa mmiliki wa kampuni ya mavazi.

kwa kuwa mama alimsimulia jinsi alichotaka kumfanyia mwanzo, wote wawili wameamua kuwa na shirika la kuwahudumia watoto waliotelekezwa na wazazi wao na pia wanatoa ushauri kwa kina dada waliopata watoto au mimba za kutotarajia kuzilea vyema kwani Mungu ana mipango na kila kitu alichowapa.

rafiki yangu unayesoma, amini kuwa hukuzaliwa kwa bahati mbaya ila ni kwa sababu maalumu, jihangaishe leo katika sehemu iliyopo na kufanikiwa ili watu waje wajue kwa nini ulizaliwa.

Kwa wenye watoto, amini ni mipango ya Mungu kuwa nao hao watoto hivyo tuwalee kwa maadili, mapenzi mema na hata kuwapa hofu ya Mungu kwani Mungu anakusudio la kukupa zawadi hizo.

Hebu firkira ni wangapi wanahangaika miaka nenda rudi na wanakosa watoto????

You Might Also Like

0 comments: