Kamwe sitasahau siku mchepuko uliponiachia mtoto kwenye daladala

05:40:00 Unknown 0 Comments

Mke wangu aliamka mapema na kuniomba niende nikamsaidie baadhi ya majukumu sokoni kwani yeye siku hiyo alikiwa akijisikia vibaya.

Hakukuwa na wakumtuma kwani tangu tuoane tuliishi sisi wawili na hatukubahatika kumpata mtoto kwa miaka zaidi ya minne ya ndoa yetu.

Nikaenda mpaka kituo cha daladala ingawa nilikuwa na mawazo mengi sana kutokana baadhi ya mambo yangu kwenda ndivyo sivyo.

Nikiwa katika dimwi la mawazo daladala iko kituo cha mbele mara mama mmoja akiwa na mtoto mchanga akaniita dirishani na kuniomba nimbebee mtoto kwani daladala ilijaa naye alihitaji kupanda.

Nilimpokea yule mtoto na baada ya pale nikamwona akizunguka upande wa pili apande nami nikaendelea kuwaza lakini safari hii nikasali kimoyomoyo kuwa Mungu anipe nami baraka ya mke wangu kuzaa.

Mawazo mchanganyiko yaliendelea kwa muda mpaka nilipokuja kugundua daladala ndio kwanza ilikuwa ikiingia kituo cha mwisho.

Nikakaa pale kusubiri watu washuke ili nimkabidhi mtoto yule kwa mama yake lakini cha kushangaza ni kwamba kila mtu alishuka na kujikuta nipo mimi na konda twaangaliana.

Nikamuuliza mama wa mtoto yuko wapi? Akadai yeye hajui wala hakuona mama mweye mtoto..

Nikamhadithia ilivyokuwa akaniambia mjomba hapo nenda polisi tu.

Polisi nikafika na kutoa maelezo nikiwa na konda pamoja na mtoto yule. Baada ya maelezo wakaniambia sasa wewe baki na mtoto na sisi twaendelea na upelelezi.

Nikaahirisha kufanya yale niliyodhamiria na kufika nyumbani mke wangu alinishangaa na hata kila nilipojaribu kuelezea hakunielewa zaidi ya kudai mtoto yule lazima awe na mahusiano nami.

Akazidi kudai kuwa lazima nimezaa na mtu na kanisusia baada ya kutomjali au anataka nioane naye au mambo mengine ambayo yawezekana kuwa ni siri za mimi na huyo mama.

Mke wangu alilia usiku na mchana kila siku nami nikazunguka huku na kule nipate njia ya kulitatua tatizo hili kwani na kwangu lilishaanza kuwa kama kidonda kibichi moyoni mwangu.

Jioni moja narudi nyumbani nikagundua kuwa mke wangu kafungasha mizigo yake na kuondoka kwenda kwao.

Ikanilazimu niende kituo kimoja cha kulelea watoto yatima nilichoambiwa kiko pale mtaani kwetu na baada ya kufika pale na kutoa maelezo wakakubali na kumchukua mtoto jambo lilofanyika ndani ya siku nne maana ilinibidi pia niende na polisi wathibitishe.

Baada ya hapo nikaanza safari kwenda kijijini kwa mke wangu.

Kufika kule baba na mama wa binti yangu wakadai kuwa kwa unyama niliomfanyia mwanao hawataniruhusu nirudiane naye tena na sasa watamruhusu aolewe na mtu mwingine.

Nililia kama mtoto mdogo nikiomba wanisamehe na kunielewa kwani mkasa huu hata mimi wanipa wakati mgumu lakini hawakuelewa.

Nikakumbuka kuwa mimi ni mhehe na wahehe tuna asili moja ya kujinyonga.

Jioni ile nikanunua kamba yangu na nilipohakikisha kila mtu kalala nikapanda juu ya mti kamba yangu singoni na kisha kujitupa chini ili kamba ile ininyonge.

Nilitapatapa pale na taratibu nikahisi haja kubwa ikinitoka kwa shida ikiashiria ndio nilikuwa nakata roho nikalia kilio cha mwisho kwa uchungu kabla ya kunaswa kibao na demu niliyelala naye guest bubu huku akinisema" mwanaume huna haya wewe mimi nakuangalia hapa warusha miguu na kujifanya kulia kumbe unakunya kitandani???????? Mwana haramu mkubwa weee?

Ndoto nyingine bwana laana tupu.

Je ungependa kuwa mdhamini wa story zetu? Chat na admin whatsapp 0713317171

You Might Also Like

0 comments: