Marafiki wa saliti kila sehemu.....
Nolesy na Mtafya ni marafiki wawili walioivana na kupendana sana tangu wakiwa wadogo mpaka walipomaliza shule na kuanza kazi wakiwa pamoja.
Mtafya yeye alifanikiwa kuwa mfanyabiashara na Nolesy yeye akabahatika kuwa wakili wa kujitegemea.
Wote walipata umaarufu katika kazi zao na wakawa wakikaa katika nyumba moja ya kupanga na kila mara baada ya kazi walionekana pamoja na hata ile mida ya chakula walikula pamoja na kisha kurudi makazini mwao.
Mwaka mmoja baadae Mtafya alifanikiwa kujenga nyumba na wote wakahamia na kuishi kwa pamoja.
Nolesy yeye alikuwa na gari na kwa kuwa hakuwa na safari nyingi zaidi ikabidi gari liwe linatumiwa na mtafya ambaye yeye alikuwa na shughuli mbalimbali za kibiashara.
Maisha yakazidi kuwa mazuri na wakasaidiana mpaka Nolesy akajenga na kuhamia katika nyumba yake na maisha yakawa mazuri na wakakubaliana kuendelea kulitumia lile gari kwa pamoja.
Haikupita muda Nolesy akaamua kumuoa rafiki yake wa miaka mingi aitwaye Habiba na harusi ilifana sana chini ya uenyekiti wa mtafya.
Maisha yakaufungua ukurasa mpya na sasa mtafya akawa lazima ale chakula cha asubuhi, mchana na jioni pale kwa Nolesy.
Na kwa kuwa gari lilikuwa likitumika na mtafya alitakiwa kumpitia asubuhi swahiba wake kwenda kazini baada ya kupata chai, mchana wakati wa chakula na jioni wakitoka kazini na baada ya mizunguko.
Kama haitoshi mara moja moja kwa kuwa Nolesy alibanwa na kazi za kimahakama hivyo mtafya alimsindikiza shemeji yake Habiba sokoni kwa ajili ya kutafuta mahitaji nyumbani na hali ile ilidumu.
Tetesi zikaanza kuenea mtaani kuwa Mtafya anatembea kimapenzi na shemeji yake na habari hizo zikamfikia Nolesy.
Nolesy hakuwa na pupa akaendelea kufuatilia mpaka siku moja saa saba mchana alipowafumania katika chumba kimoja cha hoteli iliyojificha ambako yeye alienda kwa shughuli za kikazi kabla ya kuwafuma baada ya kuliona gari lake na begi ya mkewe ikiwa kwenye siti ya mbele bila wao na kisha kumwomba mhudumu ampeleke akidai ana ahadi nao.
Nolesy baada ya kuwafumania hakusema kitu zaidi ya kuwasalimia kisha akarudi mpaka pale ofisini akamalizana na mwenyeji wake kisha akarudi zake nyumbani.
Huku nyuma mtafya na habiba jasho likawa lawatiririka wasijue nini cha kufanya.baadae wakaamua kuondoka zao mpaka karibu na kwa Nolesy kisha akamshusha habiba na habiba kwa upole akaingia nyumbani.
Akamkuta Nolesy akiwa kashaandaa chakula na kamwekea maji ya kuoga na kumwomba mke wake akaoge na akaja wakala na Nolesy akawa kama kawaida bila kumuuliza kitu na uchangamfu ule ule.
Hali ile ilidumu kwa siku kadhaa kabla ya habiba kukimbilia kijijini kwao kwa baba na mama yake ambako hakuongea kitu kwa aibu na hofu.
Siku chache baadae Nolesy akamfuata na kumrudisha nyumbani bila ya kuwaambia wazee nini kilitokea hata pale habiba alipolazimishwa aombe msamaa yeye alisema hajakosewa.
Zikapita wiki kadhaa tangu warudi mjini na ikawa ni siku nyingi tangu Mtafya waonane na Nolesy pale hotel akiwa na mkewe, hivyo ikambidi Nolesy amwambie habiba waende kwa mtafya.
Kufika pale wakaona ni kama nyumba haina mtu kwani gari lilikopaki ni kama halijaondolewa kwa siku kadhaa na kuingia ndani wakamkuta Mtafya akiwa kalala kwenye sofa na inaonyesha huwa hatoki zaidi ya kula mikate na chupa za bia zilizozagaa pale ndani.
Kuwaona tu akaanza kulia na kumwomba msamaha Nolesy kwa kutembea na mke wakati wao walikuwa marafiki.Nolesy akasema nimekusamehe na nilishasahau ila nimemleta huyu akae akusaidie maana inaonyesha huwa huli hapa wala kufanya kazi.
Habiba alitaka kukataa lakini alisalimu amri baada ya Nolesy kuonyesha hana masiara. Na kumwambia kuwa kama itatokea siku naye mtafya akasalitiwa na habiba kamwe asimdhuru na kuwa kimya kama yeye Nolesy alivyowafanyia na kisha akaondoka.zake na kuwaacha.
Zikapita siku, mara miezi huku mtafya akiwa anakaa na habiba kama mke wake na Nolesy akiendelea na kazi zake za kila siku akiwa na furaha na kampata mchumba mpya aitwaye Rehema.
Siku moja Mtafya akawa anasafiri kutoka pale mjini kwenda kijijini kuangalia miradi yake. Kufika njiani akapata tatizo la gari, ikambidi aliache gari pale na fundi ili yeye arudi nyumbani kuchukua gari lingine ili aendelee na safari.
Kufika nyumbani kwake akaona mlango uko wazi na kuingia moja kwa moja mpaka chumbani na kuona habiba akiwa na rafiki yake aitwaye Salva wanakula tunda la mtu wa kati kati.
kwa hasira akachukua kisu na kumchoma Salva na kelele za habiba zikawaita majirani na kuja pale kabla ya Mtafya kuchukuliwa na kupelekwa polisi kwa kesi za kumuua mgoni wake.
Habari zile zikamfikia Nolesy ambaye akatumia nguvu na uwezo wake wa kitaaluma mpaka Mtafya akaachiwa huru na mahakama kwa kuua bila kukusudia na kurudi uraiani baada ya kukaa mahabusu kwa zaidi ya mwaka na nusu.
Baada ya kutoka mtafya akajiuliza maswali mengi:
1. Nilitembea na mke wa Nolesy na kuusaliti urafiki wetu na akaniacha huru bila kunidhuru.
2. Nikakaa kwa msongamano wa mawazo akaja na kuniambia amenisamehe
3. Nimeua baada kumfumania mtu na mke wangu na bado akajituma na kunitoa na niko uraiani...... Ananitakia nini mimi NOLESY?????????
BAADA YA KUTOPATA MAJIBU YA MASWALI HAYO HATIMAYE MTAFYA ALIAMUA KUJINYONGA
0 comments: