Kamwe usiipite habari hii bila kumsaidia ushauri huyu dada yetu
Mimi ni binti wa miaka 29 na nilihitimu elimu yangu ya chuo kikuu miaka mitano iliyopita.
Nilisomea masomo ya biashara na baada ya kuhitimu kwa kuwa sikuwa na uzoefu wa kutosha nikabahatika kuajiriwa na kampuni moja mpya.
Makubaliano yalikuwa ni kupata ujira mdogo na marupurupu yalitegemeana na wateja utakaowapata na kujiunga na kampuni yetu wakiwa wanunuzi au wateja wa huduma zetu.
Nilipata wakati mgumu kuwapata wateja na kwa kuwa nina shida ya kazi nikajikuta nimeanza kunasa katika mitego ya baadhi ya wateja ambao walinitaka kimapenzi kwa ahadi za kuwa wateja na kunipa fedha mimi.
Maisha yaliendelea hivyo na nikafanikiwa kutafuta mtaji wa mama na kuanza biashara yake na mimi nikaanza kujenga nyumba na kulipia karo za wadogo zangu.
Mwaka jana mwishoni nikapimwa baada ya kuumwa vidonda vya koo na fangasi zisizo za kawaida na hatimaye kukutwa nimeathirika.
Mpaka sasa ni miezi minne sina kazi na nimekonda sana na siwezi kuongea zaidi ya kutumia ishara kwani fangasi hao wamenishambulia sana naogopa mama yangu asije jua nimeathirika kwani ataweza kufa kwa presha kwa jinsi anavyonitegemea kwa sasa katika familia yetu.
Naogopa pia kuanza matibabu kwani ataelewa kwa haraka, nimejaribu kutaka kujiua zaidi ya mara nne ila mama yeye anafikiri mimi nina kichaa baada ya homa kunizidia.
Sina wa kunishauri ila kwa wewe unayesoma naomba ushauri wako kama utaumia na hali yangu ambayo imetokana na jitihada zangu za kuiokoa familia kwani kuna wakati tishatolewa nje ya nyumba na kunipa mimi maamuzi ya kuanza kuwa na tabia hii.
Najua ni mkosaji ila naomba nisamehewe kwa hukumu yoyote na nipate ushauri kwani sasa hata watu jirani siongei nao kwa kuwa fangasi wameniathiri na kunifanya nionekane kituko na mbaya sana kuchekwa na kukimbiwa na hata wale marafiki wa karibu.
Ndugu yangu unayesoma habari hii naomba ushauri wako wenye kunijenga na kunipa tumaini jipya.
Asante
kama umeguswa share ushauri wako HAPA

0 comments: