HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU " Season 12
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Season 12
ILIPOISHIA
Kesho yake asubuhi nilijiandaa na kuelekea kazini wakati nipo njiani meseji ikaingia iliyosema, " Kaka umelalaje?" sikujibu kwa hasira nikajua ni baba pachu aliyeniletea kesi na kujifanya kunijulia hali, nikaendelea na safari kwenda kazini.
Nilipofika kazini secretary aliniletea kinoti kalichokuwa na ujumbe ndani yake ulionitaka .............................. .............................. ..............................
Endelea
NILIPOFIKA kazini secretary aliniletea kinoti kalichokuwa na ujumbe ndani yake ulionitaka baada ya kazi jioni nikutane na mtu huyo aliyedai nitamtambua pindi nitakapo onana nae.
Sikujali sana maana kutokana kazi yangu vikao vya namna hii huwa havikwepeki kwani kuna baadhi ya wateja hupenda kukufanya kama rafiki ili uwafahamishe zaidi kuhusu huduma zetu kabla ya kufikia uamuzi wa kuzitumia.
Nilimaliza kazi mapema siku hiyo na kuanza safari ya kwenda kwenye hoteli hiyo ili nikutane na huyo mtu na kuwahi kurejea nyumbani hasa ukizingatia jana yake sikulala usingizi wa kawaida kutokana na ile simu ya mwana dada nayeonekana kuwa gaidi.
Nilitumia muda mrefu njiani hasa ukizingatia siku hizi pale mafyati foleni yake ni kama tuko Dar vile lakini baada ya kitambo nikawa nimewasili pale hotelini. Nilijivuta na kuchukua kiti na kukaa sehemu moja ya wazi na kisha nikaagiza kinywaji na kuanza kunywa.
Zilipita dakika kadha pale bila ya kuona dalili ya mtu yoyote kuja, nikazidi kumsubiria kwa muda kabla ya ujumbe mfupi wa maneno kuja kwenye simu yangu na kusomeka hivi,. " Ukiambiwa uwahi sehemu uwe una wahi na sio vinginevyo"
Nilishangaa iweje mtu aniombe nije na aanze kuongea kwa utemi? Kweli dunia ina mambo. Nikanyanyuka na kuondoka ila wakati huu nilikasirika sana na kuona kuwa kuna watu wana utani na muda wa watu.
Sikuitazama kwa makini ile namba ila baada ya kuichunguza wakati naondoka nikagundua ni namba ya yule dada aliyenipigia simu jana yake usiku.
Kwa taharuki nikaitupa ile simu chini na kuanza kushika kichwa kila mtu akawa sasa ananiangalia mimi pale hotelini..... Nikaiokota na kuzuga kwa sauti " Yaani hizi simu za kichina bwana zimezidi eti sasa zimeanza kupiga shoti"
Nilijikaza na kuingia garini na kuanza kuondoka kurudi nyumbani lakini ilinichukua dakika kumi na tano kuja kugundua kuwa nilikuwa naelekea barabara ya chunya badala ya kwenda barabra ya kurudi nyumbani kwangu mbalizi.
Nikageuza gari na kuanza kurudi nyumbani ila sikufika nyumbani kabisa nikaingia bar ya jirani ili niweze kupata kinywaji kikali na kutafakari kuwa haya sasa yaliyopo mbele yangu ni maigizo au kuna ukweli ndani yake? Na kama kuna ukweli ni kwanini huyu mtu asinifuate na kuongea??????
Nilikaa pale bar na nakumbuka nilipiga bia tatu na mizinga miwili midogo ya konyagi na baada ya kuona sasa naanza kupoteza fahamu na ujasiri wa kurudi kulala unaninyemelea nikamwita mhudumu anipe bili yangu.
Mhudumu akaja na bili lakini wakati naikagua kagua upande wa pili kuliandikwa,
" Unakimbilia pombe ukidhani ni suluhisho? Mimi na wewe lazima tuongee" na chini yake kulikuwa na namba ya yule binti.
Moyo uliruka kama mmasai aliyepandisha mori baada ya kuambia dawa zake ni feki. Badala ya kukimbia kwenda mlango wa gari nikawa nakimbilia kwenda mlango wa choo cha kike pale bar, kilchonifanya nigundue naingia mlango ambao haunihusu ni baada ya mhudumu kusema,
"wewe kaka unaenda wapi huko?"
Nikamtania kuwa nilikuwa nataka kuona kama wafanyakazi wa hapa mko makini ila umenifurahisha uko makini sana nitakuajiri, kisha nikamlipa fedha zake na kuanza kuondoka kurudi nyumbani ingawa pombe zilishaniishia nikafika nyumbani na kujilaza kitandani.
Nilipitiwa na usingizi na kuja kushtushwa na mlio wa simu ambao niliusikia na kujifanya sijausikia maana nilihisi kuna jambo. Iliita zaidi ya mara tatu nikaona isiwe taabu nikasimama na kwenda kuifuata sebuleni.
Kupokea kumbe alikuwa ni secretary akiniambia mbona umechelewa kuna kikao unasubiriwa wewe, kutazama saa ilikuwan ni saa sita kasoro nikakurupuka na kuingia bafuni kisha nikajiandaa na kwenda haraka kazini.
Nilipofika pale nikasalimiana na watu, katikati ya kikao simu iliita nikaomba nitoke nje ili niipokee. Daah daaah daah haki ya nani hii simu ilinifyanya .............................................................................
Je simu hiyo ilikuwa na ujumbe gani au ilinitaka nifanye nini?
Usikose kisa hiki kesho jioni
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu kwa udhamini wa Gracious HOUSE of CAKES watengenezaji maarufu na waliobobea wa keki za aina mbalimbali kwa hafla mbalimbali waliopo jijini Mbeya na wanapatikana kwa namba 0767218014
Nawe waweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo
share, like na comment
Kama ni mkazi wa jiji la MBeya na vitongozi vyake HII si ya kuikosa (bofya neno hii kuona yaliyomo)
0 comments: